December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe: Kitabu cha kumbukumbu mahabusu chaibua mjadala

Spread the love

 

KITABU cha kumbukumbu za mahabusu (DR), cha Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, kimeendelea kuibua mkanganyiko katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mkanganyiko huo umeibuka leo Jumatatu, tarehe 22 Novemba 2021 mahakamani hapo mbele ya Jaji Joachim Tiganga, wakati shahidi wa pili wa jamhuri, Askari Mpelelezi, DC Ricardo Msemwa, akihojiwa na mawakili wa utetezi kuhusu kitabu hicho.

Ni baada ya kitabu hicho cha mahabusu chenye taarifa zinazodai washtakiwa wenzake Mbowe, Adam Kasekwa na Mohammed Ling’wenya, walikuwa kituoni hapo tarehe 7 Agosti 2020, kupokelewa kama kielelezo cha ushahidi wa jamhuri kwenye kesi ndogo ya kupinga maelezo ya onyo ya Ling’wenya yasipokelewe mahakamani hapo.

Mkanganyiko wa kwanza uliibuka baada ya Wakili Peter Kibatala, kumuuliza mwaka ambao kitabu hicho kilijazwa taarifa za washtakiwa hao.

Mahojiano yao ilikuwa kama ifuatavyo;

Wakili Kibatala: Hiki kielelezo kilianza kujazawa tarehe ngapi?

Shahidi: Sikumbuki

Wakili Kibatala: Naomba usome (DR), kilianza kujazwa tarehe ngapi?

Shahidi: Tarehe 24 Julai 2020

Wakili Kibatala: Entry(ingizo) ya Lin’gwenya inaanza au mwanzo au iko mbele?

Shahidi: Iko mbele

Wakili Kibatala: Hii imeacha kutumika tarehe ngapi?

Shahidi: Imeacha kutumika tarehe 12 Agosti 2020

Wakili Kibatala: Mwambie Jaji entry (ingizo) namba  310 inaonekana hiyo 2021 ni nini?

Shahidi: Hii sijui inahusiana na nini

Wakili Kibatala: Fungua Entry namba 208 umeona tarehe ngapi? Tarehe  4 Agosti mwaka gani?

Shahidi: Haisomeki

Wakili Kibatala: Hii 2021?

Shahidi: Haisomeki

Wakili Kibatala: Mwaka gani (anamuonesha DR)?

Shahidi: Hii haisomeki

Wakili Kibatala: Mimi  najua ni 2021 wewe unajua  mwaka gani?

Shahidi: Haisomeki

Wakili Kibatala: Fungua entry 114, hii Julai mwaka gani?

Shahidi: Mwisho wameandika 21

Wakili Kibatala: Mwaka gani iliacha kutumika?

Shahidi: tarehe 12 Agosti 2020

Wakili Kibatala: Nenda entry namba 113, tarehe 30 Julai mwaka gani?

Shahidi: Hii haisomeki

Wakili Kibatala: Hii  21 ni nini?

Shahidi: Haioneshi mwaka

Wakili Kibatala: Fungua entry  156 tarehe 2 Agosti mwaka gani? Mwisho ina maanisha mwaka gani?

Shahidi: Inamaanisha mwaka 2021

Wakili Kibatala: Hiki kielelezo kinapima ukweli na uongo wake unafahamu?

Shahidi: Nafahamu kama kinapimwa

Wakili Kibatala alimhoji Askari Msemwa kuhusu sababu za kuwatoa wa tuhumiwa hao zilizodaiwa kuandikwa katika kitabu hicho kama ifuatavyo;

Wakili Kibatala: Nilisikia mkiulizana na Wakili John Mallya sababu za kumtoa Ling’wenya ilikuwa nini?

Shahidi: Ni nje kwa upelelezi

Wakili Kibatala: Na unasema nje kwa upelelezi  inajumuisha nini?

Shahidi: inajumuisha vitu vingi ikiwemo mchakato mzima wa kuanzia kesi, hadi  kuifikisha mahakani.

Wakili Kibatala: Elezea wapi ulifafanua  kwamba hapa alitolewa nje kwa upelelezi lakini hapa ilikuwa naamanisha nje kwa upelelezi inajumuisha kuchukua maelezo ulimwambia?

Shahidi: Mahojiano ni  sehemu ya upelelezi nilitaja

Wakili Kibatala: Kutolewa nje kwa upelelezi na kutolewa nje kwa  mahojiano ni sawa?

Shahidi: Sawa

Wakili Kibatala: Kwa kusoma  nje kwa mahojiano na upelelezi zinafanana?

Shahidi: Hazifanani lakini ni maana moja

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla, alimtaka atoe ufafanuzi kuhusu utofauti huo kama ifuatavyo;

Wakili Hilla: uliulizwa swali kuhusiana na zile sababu za watu kutolewa nje mahabusu, ukasema kwa mahojiano na upelezi, ifafanulie mahakama ulikuwa na maana gani?

Shahidi:  Kutolewa nje kwa  mahojiano nina maana mtuhumiwa anatolewa specific  kwa kuhojiwa.

Wakili Hilla: Sababu ya watu kutolewa kuna mahala uliulizwa kwa kusoma maneno tofauti, ukajibu ulimaanisha nini?

Shahidi: Nilimaanisha kwa kusoma neno mahojiano na  upelelezi ni tofauti lakini mahojiano inaingia katika upelezi lakini mahojiano ni sehemu ya upelelezi.

Kada wa Chadema adai alimkuta  Kituo cha Polisi Oysterbay badala ya Kituo Kikuu cha polisi Dar es Salaam.

Wakili Kibatala alimuuliza Msemwa kama anamkumbuka mwanachama  wa Chadema aliyekuwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay.

Wakili Kibatala: Kuna mtu anaitwa Lembrus Mchome unamfahamu huyu mwanachama wa Chadema, alikamatwa kwa tuhuma za kupiga picha gari ya kiongozi wa usalama alikuwa kizuizini Oysterbay unamkumbuka?

Shahidi: Simkumbuki

Wakili Kibatala: Yeye anasema Mei 2020 wewe ulikuwa Oysterbay na wewe binafsi ulimpokea ukiwa CRO duty (Afisa wa Chumba cha Mashtaka) Oysterbay  2020 wewe unasemaje?

Shahidi: Sikumbuki na pia sikuwepo Oysterbay kwa wakati huo

Wakili Kibatala: Anaweza kuwa na sababu gani za kusema uongo kuhusu wewe?

Shahidi: Sijajua sababu zake ni zipi

Wakili Kibatala: Una ugomvi naye?

Shahidi: Wala simfahamu simjui na sijui sababu ya yeye kusema uongo au kusema ukweli.

Wakili Kibatala: Tukimleta sisi kama shahidi wakati Ling’wenya anajitetea utasemaje?

Shahidi: Atasikilizwa na jaji

Ahojiwa kuhusu diary

Wakili Kibatala: Unafahamu diary uliyokutwa nayo kwenye kizimba  kurasa mahsusi zinazohusiana na maeneo tuliyoangiza  mahakamani unafahamu?

Shahidi: Sifahamu

Wakili Kibatala: Wakati mahakama inafanya maamuzi hukusikia wakati tunafanya maombi diary ichukuliwe na zile kurasa tunazotaka zichukuliwe ulikuwa kwenye kizimba?

Shahidi: Sikuwa kwenye kizimba

Wakili Kibatala: Ulikuwa uko wapi?

Shahidi: Mahakamani

Wakili Kibatala: Wapi tuoneshe?

Shahidi: Sikumbuki mheshimiwa jaji nilikuwa wapi, kama sio chumba cha nanii kule nilikuwa ndani

Wakili Kibatala: Angalau unafahamu kwamba diary yako ulikuwa nayo kuna kurasa fulani zinahusu kufanya ushahidi wako pamoja na kuomba iingie kwenye rekodi ya mahakama unafahamu?

Shahidi: Vitu vinavyohusiana kwenye shauri hii viko kwenye diary yangu?

Wakili Kibatala: Ndio vipo

Wakili Kibatala: Mwambie jaji kabla hujakabidhiwa kwetu kwa ajili ya cross examinatiom uliongozwa na jamhuri kufafanua chochote kuhusiana na kidhibiti namba moja (diary) ambapo ndani yake kuna vitu vinahusiana na ushahidi wako?

Shahidi: Hillo sijafafanua.

error: Content is protected !!