December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe: Jaji mpya ajitambulisha, RPC Kingai aanza kutoa ushahidi

Spread the love

 

KESI inayomkabili Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, imeanza kusikilizwa tena katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Halfan Hassan Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Abdillah Ling’wenya.

Kesi hiyo ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi, imeanza leo Jumanne, tarehe 26 Oktoba 2021, mbele ya Jaji mpya Joackim Tiganga aliyepewa jukumu la kuisikiliza, baada ya kujitoa kwa Jaji Kiongozi Mustapha Siyani.

Siyani alijitoka kusikiliza ikiwa ni siku chache zimepita tangu Rais Samia Suluhu Hassan, alipomteua kuwa Jaji Kiongozi, hivyo kusema kwamba kwa majukumu hayo asingeweza kuendelea nayo.

Kabla ya kuanza leo Jumanne, Jaji Tiganga ameanza kwa kusema “tarehe 20 Septemba wakati Jaji Siyani akitoa amri ya kujitoa alisema jaji mwingine atakuja na jaji mwemyewe ndiyo mimi.”

“Kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jina ya 2019, napenda kuwataarifu kwamba naendelea na shauri hili kwa sababu ambayo jaji aliyekuwa akisikiliza alizitoa wakati akijitoa. Kwa sababu hiyo, shauri litaendelea kwa kuruhusu jamhuri kuleta shahidi wake,” amesema Jaji Tiganga

Mara baada ya kueleza hayo, upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili mwandamizi Robert Kidando kuieleza wanaweza kuendelea na ushahidi na tayari shahidi Kamanda wa Polisi Kinondoni, ACP Ramadhan Kingai yupo mahakamani.

Jaji Tiganga akatoa maelezo kwamba aitwe na akaitwa kuanza kutoa ushahidi kwa kusoma maelezo ya onyo ya mshatiwa Adam Kasekwa.

Awali, kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, Peter Kibatala alisema, mawakili sita akiwemo na yeye, watamtetea Freeman Mbowe huku mshtakiwa wa kwanza na wa tatu katika kesi hiyo, wakiwakilishwa na mawakili wawili na wa pili akiwakilishwa na mmoja.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kimajii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!