November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe: Hatima shahidi aliyekuwa na ‘diary’ leo

Spread the love

MAHAKAMA Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, leo Jumanne, tarehe 16 Novemba 2021, itatoa uamuzo mdogo wa pingamizi la utetezi la kumkataa shahidi wa Jamhuri, Ricardo Msemwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya rushwa, inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Pingamizi hilo, liliwekwa Ijumaa iliyopita tarehe 12 Novemba 2021, baada ya upande wa utetezi kudai, shahidi huyo wa pili kwenye kesi ndogo, Msemwa alikutwa na simu, kalamu na diary akiwa kizimbani.

Msemwa ambaye na polisi wa kituo cha Oysterbay alikuwa akitoa ushahidi katika kesi ndogo ya kupinga maelezo ya onyo ya Mohamed Ling’wenya yasipokelewe mahakamani hapo.

Jana Jumanne, mawakili wa pande zote, waliitumia kuchuana vikali kisheria kwa kila mmoja, kutetea hoja zake. Utetezi wanadai shahidi huyo wa Jamhuri amekosa sifa kwa kukutwa na vifaa hivyo huku upande wa mashtaka ukidai pingamizi hilo halina uzito.

Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo, ndiye anatakayetoa uamuzi huo.

Mbali na Mbowe kwenye kesi hiyo ya aina yake wengine ni, Halfan Hassan Bwire, Adam Kasekwa na Mohammed Abdilah Ling’wenya.

Bwire, Kasekwa na Ling’wenya walikuwa makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kikosi cha Ngerengere mkoani Morogoro.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!