January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe: Hakimu amkunjulia makucha DPP

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, imeitaka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kuharakisha taratibu za uendeshaji mashtaka ya uhujumu uchumi na kula njama za kufanya ugaidi, yanayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo, Freeman Mbowe na wenzake watatu. Anaripoti Regina Mkonde. Dar es Salaam … (endelea).

Amri hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 6 Agosti 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba, baada ya upande wa Jamhuri kuomba kesi hiyo iahirishwe kwa madai DPP hajakamilisha taratibu zitakazowezesha kesi hiyo, kuhamishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Mbowe na wenzake watatu ambao ni, Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohammed Abdillah Lingwenya, wanakabiliwa na mashtaka sita.

“Inatakiwa tuwe na consistence (uthabiti) ya proceeding (kuendelea) na kesi. kuna issue (suala) la ku-file information, nataka tupate taarifa kamili kama haijakamilika kwa sababu ya upelelezi. Katika hii kesi yale tunayopanga yawe haraka, sababu kesi hii ni kubwa,” amesema Hakimu Simba na kuongeza:

“Hoja ya Kibatala inaweza kuwa ya msingi ingawa siwezi sema ni sahihi. Mmesema faili liko kwa DPP inasubiri ku-file (kufunguliwa). Tarehe 19 Agosti 2020, washtakiwa wako ndani, kwa maana hiyo, Tujitahidi ku-comply na mashrati ya kisheria.”

Awali, Wakili wa Serikali, Pius Hilla, aliomba kesi hiyo iahirishwe kwa madai kuwa DPP hajakamilisha baadhi ya taratibu. Hata hivyo, alidai kwamba upelelezi wa kesi hiyo imekamilika.

“Kinachosubiriwa ni DPP kuwasilisha jalada kwenye mahakama inayotakiwa kusikiliza kesi. Lakini upelelezi umekamilika,” alidai Hilla.

Taarifa hiyo ilipingwa na Peter Kibatala, anayeongoza jopo la mawakili wa utetezi, aliyetaka kesi hiyo iharakishwe kusikilizwa, kwa madai washtakiwa hawataki kujua kinachoendelea katika ofisi ya DPP.

Kibatala aliiomba mahakama hiyo iendeshe kesi hiyo haraka, kwa kuwa DPP alisema upelelezi wake umekamilika.

error: Content is protected !!