Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe: Fuatilia mtaalamu wa silaha akitoa ushahidi, milipuko  
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe: Fuatilia mtaalamu wa silaha akitoa ushahidi, milipuko  

Spread the love

 

KOPLO Hafidh Abdallah Mohamed, mwenye namba F 5914 D ambaye ni shahidi wa tatu upande wa Jamhuri, ameanza kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni leo Ijumaa tarehe 29 Oktoba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iliyopo Mawasiliano jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joackim Tiganga.

Mbowe na wenzake – Halfan Hassan Bwire, Adam Kasekwa (Adamoo) na Mohamed Abdillah Ling’wenya – ambao walikuwa makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kupanga njama za ugaidi.

Koplo Mohamed anaendelea kutoa ushahidi wake baada ya kukamilika mashahidi wawili ambao ni Kamanda wa Polisi wa Kinondoni (RPC), Ramadhan Kingai pamoja na Justine Elia Kaaya ambaye alikuwa msaidizi wa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Koplo Hafidhi ameanza kutoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla, mahakamani hapo.

Ameileza mahakama hiyo, anafanya kazi makao makuu ndogo ya jeshi la polisi Dar es Salaam, kitengo cha matumizi ya silaha na milipuko, tangu mwaka 2004.

Amedai majukumu yake ni kuchunguza silaha, risasi na maganda, vifaa vinazotuhumiwa kufanyia uhalifu na milipuko.

Askari huyo amedai, majukumu yake mengine ni kuandaa ripoti ya kitaalamu kuhusiana na kesi mbalimbali ambazo zimechunguzwa.

Sehemu ya mahojiano;

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na leo tuna shahidi mmoja. Tupo tayari kuendelea.

Jaji: Upande wa utetezi?

Wakili Peter Kibatala: Na sisi tupo tayari kuendelea.

(Jaji anaandika)

Jaji: Na anakuwa shahidi namba ngapi?

Wakili wa Serikali: Namba tatu.

Jaji: Apande [kizimbani].

Jaji: Majina?

Shahidi: Namba F 5914 D Koplo Hafidh Abdallah Mohamed.

Jaji: Umri?

Shahidi: Miaka 38.

Jaji: Kazi.

Shahidi: Askari Polisi.

Jaji: Dini?

Shahidi: Muislamu.

Shahidi: Mimi namba F5914 Koplo Hafidh, naapa kuwa kwa ushahidi huu nitakaotoa utakuwa wa kweli. Eeeh Mwenyezi Mungu nisaidie.

Jaji: Kiapo kiko sawa? Asaidiwe.

Shahidi: Mimi Koplo Hafidh nathibitisha kuwa ushahidi nitakaotoa utakuwa wa kweli, kweli mtupu, Eeh Mwenyezi  Mungu nisaidie.

Wakili wa Serikali: Nitakuuliza maswali utajibu kwa sauti.

Wakili wa Serikali: Itaje kazi yako.

Shahidi: Ni askari Polisi. Nafanya Makao Makuu Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali: Askari polisi tangu lini?

Shahidi: Tangu mwaka 2013.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama tukufu kituo chako cha kazi ni wapi.

Shahidi: Forensic Bureau Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali: Forensic Bureau ni kitu gani?

Shahidi: Ni maabara ya uchunguzi wa kisayansi.

Wakili wa Serikali: Upo kitengo gani?

Shahidi: Silaha na milipuko.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama kitengo chako kinahusika na nini (ballistic and explosion).

Shahidi: Uchunguzi wa silaha na milipuko.

Wakili wa Serikali: Upo tangu lini?

Shahidi: Tangu mwaka 2004.

Wakili wa Serikali: Umesema kitengo chako kinahusika kuchunguza silaha. Eleza majukumu yako ya msingi ni yapi.

Shahidi: Kuchunguza silaha zinazotumiwa kufanya uhalifu.

Wakili wa Serikali: Kingine?

Shahidi: Kuchunguza risasi ambazo zinatuhumiwa kufanya uhalifu.

Wakili wa Serikali: Jingine?

Shahidi: Kuchunguza maganda ya risasi.

Wakili wa Serikali: Jingine?

Shahidi: Kuchunguza kitako cha risasi.

Wakili wa Serikali: Jingine?

Shahidi: Kwenda eneo la tulio kwa uchunguzi.

Wakili wa Serikali: Jingine?

Shahidi: Kuandaa report baada ya kuchunguza ballistic and explosion report.

Wakili wa Serikali: Jingine?

Shahidi: Kutoa ushahidi mahakamani.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama kama una jukumu lingine.

Shahidi: Hakuna.

Wakili wa Serikali: Kuna uchunguzi wa silaha wa aina ngapi?

Shahidi: Aina mbili.

Wakili wa Serikali: Aina ya kwanza?

Shahidi: Physical examination.

Wakili wa Serikali: Mnafanya mambo gani?

Shahidi: Kupokea silaha mbalimbali zinazofanya uhalifu. Je, hii silaha inafanya kazi? Hii silaha ni nzima? Hii sasa ni Physical Examination.

Wakili wa Serikali: Sasa mnafanya nini?

Shahidi: Tunafanya Visual Examination.

Wakili wa Serikali:  Ni kitu gani hapo?

Shahidi: Hii bunduki ni nzima? Ina koki? Ina magazine? Je, magazine ni nzima? Kama inagonga vizuri kama nyundo? Ina nguvu? Nita ikoki katika upande wa mitambo kama inafanya vizuri. Je, fine pin inafanya kazi?

Jaji: Fine pin  ni nini?

Shahidi: Kiwashio cha risasi.

Shahidi: Nitaangalia ndani ya bao (mtutu) internal ballistic.

Shahidi: Nitaangalia ni safi? Nitaikoki kama inafanya vizuri. Ni hayo tu.

Wakili wa Serikali: Sasa uchunguzi wa aina ya pili ni upi?

Shahidi: Nimepokea pistol au SMG.

Wakili wa Serikali: Unaitwaje huu uchunguzi wa pili?

Shahidi: Comparison Examination.

Wakili wa Serikali: Kitu gani kinafanyika?

Shahidi: Nachukua ganda nililoletewa na mteja kisha napeleka kwenye mitambo maalumu.

Wakili wa Serikali: Unafanya hii comparison kubaini nini?

Shahidi: Je, hii risasi ina sifa hii?

Wakili wa Serikali: Mnatumia mitambo maalumu?

Shahidi: Unaitwa Computer Microscope and Digital Camera Forensic Machine LAECA 2004.

Wakili wa Serikali: Umeeleza za vyema kuhusu uchunguzi wa silaha. Kwenye risasi unafanya kitu gani?

Shahidi: Kitaalamu inaitwa live ammunition. Nitaangalia kiwashio. Je kimegongwa? Kama kimegongwa hiyo siyo nzima. Hiyo tunasema miss-fired. Kwamba ilipigwa na haikulipuka. It was miss-fired.

Wakili wa Serikali: Na hiyo miss-fired ieleze Mahakama. Je, live ammunition ikiwa miss-fired maana yake ni nini?

Shahidi: Ni mbovu sababu ulipiga haikulipuka.

Wakili wa Serikali: Fafanua sasa Mahakamani endapo haijagongwa ni vipi?

Shahidi: Kama haijagongwa ni nzima.

Wakili wa Serikali: Tofauti na kugomgwa na kutokugongwa mnafanya kitu gani?

Shahidi: Tunaangalia gun powder resolutions.

Wakili wa Serikali: Mnaangalia kitu gani?

Shahidi: Kwemye risasi kuna powder. Tunaangalia je, powder yako imeganda au nzima?

Wakili wa Serikali: Sasa tunataka kwenye risasi. Mnasema mnachunguza maganda ya risasi?

Shahidi: Tunachunguza pin impression (mapigo ya bunduki). Je, yanalingana?

Wakili wa Serikali: Ulisema mnachunguza vichwa vya risasi?

Shahidi: Yani bullets cartridge. Tunaangalia michirizo, yaani Internal Ballistics. Hizo alama za kipekee tunasema proved.

Wakili wa Serikali: Mnafanyaje?

Shahidi: Tunaangalia kitu kinaitwa Twist. Twist silaha/risasi kuna twist right na twist left. Naangalia counts inasema twist right na left. Nyingine unapopiga kuna counts mbili unapopiga mpaka kumdhuru mtu.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama mnamo tarehe 25 Novemba unakumbuka ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa ofisini kwangu Makao Makuu madogo Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali: Ulikuwa wapi?

Shahidi: Kwenye dawati la kupokea vielelezo mbalimbali.

Wakili wa Serikali: Ulipokea vielelezo vipi siku hiyo?

Shahidi: Nilipokea vielelezo kutoka Ofisi ya DCI ambavyo ni pistol yenye namba A5340 caliber 9mm ikiwa na magazine yenye rangi nyeusi na nikapokea risasi tatu.

Wakili wa Serikali: Za silaha gani?

Shahidi: Za pistol caliber 9mm.

Wakili wa Serikali: Vielelezo hivyo viliambatana na nini?

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

Habari MchanganyikoTangulizi

Baba aomba msaada kuzika miili ya familia yake iliyofunga bila kula kuonana na Mungu

Spread the loveWAKATI Mamlaka nchini Kenya, ikiendelea kukabidhi miili ya watu waliofariki...

Habari za Siasa

Rais Samia ampongeza mpinzani aliyeshinda urais Senegal

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mwanasiasa wa...

error: Content is protected !!