Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe: Chadema yalia na JPM, AG, DPP
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe: Chadema yalia na JPM, AG, DPP

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinaimani kuwa, kuzuiwa kwa dhamana ya Mwenyekiti wake wa Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini kinakwenda kinyume na taratibu za kimahakama. Anaandika Regina Mkonde … (endelea).

Ni kutokana na kuondolewa kwa notisi iliyopelekwa na serikali katika Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza rufaa ya viongozi hao.

Chama hicho kimemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati sakata la kunyimwa dhamana Mbowe na Matiko katika kesi inayowakabili kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 5 Desemba 2018 jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara, John Mnyika amemwomba Rais Magufuli kutoa maelekezo ya kesi hiyo kufutwa pamoja na kuondolewa kwa notisi iliyopelekwa na serikali katika mahakama ya rufaa.

Mnyika amedai kuwa, kitendo cha Mbowe na Matiko kuendelea kusota rumande baada ya kufutiwa dhamana na mahakama hiyo, kinaashiria kwamba kauli aliyoitoa Rais Magufuli wakati akifungua maktaba ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hivi karibuni, imeanza kutekelezwa.

“Tunatoa wito kwa Rais Magufuli, Waziri wa Katiba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), kama hawa wanasheria wa serikali hawajatumwa na wao na wanaona kama rasilimali na muda wa mahakama unapotezwa atoe agizo kama alivyotoa agizo katika uzinduzi wa maktaba ya UDSM.

Afikishe ujumbe kwa Nchimbi na Kadushi waache kutumia rasilimali za mahakama vibaya waondoe notisi katika mahakama ya rufaa.Atoe maelekezo kesi ifutwe na notisi iondolewe isipofanywa hivyo tutaendelea kuamini kauli yake ya kufurahia viongozi wa upinzani kwenda magerezani kama hatoingilia kati suala hili,” amesema.

Katika hatua nyingine, Mnyika amesema Chadema inaoiomba mahakama ya rufaa kufanya marejeo ya faili la shauri lililoko katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu ili kujua mwenendo wa shauri hilo kwa minajili ya kutoa haki.

“Mahakama kabla ya kwenda likizo tarehe 15 Desemba 2018, tunaiomba mahakama ya rufaa kuita pande zote mbili, kufanya mapitio ya faili la kesi ya Kisutu na mahakama kuu. Tunajua mahakama ya rufaa ina vikao katika mikoa mingine, tuko tayari popote tutakapoitwa kwenda kwa umuhimu na dharula ya shauri hili ili kutafuta haki,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!