Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe: Askofu Mwamakula awapa mbinu Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe: Askofu Mwamakula awapa mbinu Chadema

Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki, Emmaus Mwamakula
Spread the love

 

KIONGOZI wa Kanisa la Uamsho la Moravian, Askofu Emmaus Mwamakula, amewataka wanachama na wafuasi wa Chama cha Chadema, kuendelea kupasa sauti zao ili mamlaka husika zimwache huru Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe na wenzake watatu, wanakabiliwa na kesi ya ugaidi katika Mahakma Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam.

Askofu Mwamakula ametoa wito huo leo Alhamisi, tarehe 9 Desemba 2021, Dar es Salaam, akizungumza katika kongamano la miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, lililoandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).

“Naomba mjitokeze kwa wingi katika kesi, nenda kusikiliza kesi ya Mbowe faida yake iko wapi? mkionesha kwa wingi ushirikiano, mkihudhuria kwa wingi hizo kesi, Serikali inasikia.”

“Niwaambie kitu kimoja, kwenye mitandao msiwe watu wakali sana mnajua mama na yeye amechoka na haya mambo na anasema hilo gari bovu sitaki liniangukie. Ninyi mkisimama mkiwa wengi si atasema namna umma wa Watanzania hawa,” amesema Askofu Mwamakula.

Askofu Mwamakula amesema, kelele za mitandao hazitasaidia kutatua tatizo hilo.

“Jitokezeni kwa wingi kupaza sauti,  mitandao ya kijamii haitoshi, hudhurieni kwa wingi katika kesi, ukisema nyumbani Mbowe sio gaidi inasaidia nini?  Siku ya tarehe 14 Desemba 2021 wanatoa uamuzi vaa t-shirt ya katiba mpya kusanyikeni wengi,” amesema Askofu Mwamakula.

Wakati huo huo, Askofu Mwamakula ameiomba Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, imfutie mashtaka Mbowe.

“Natoa wito kwa Serikali ya CCM  inayoongozwa na Rais Samia katika miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa upinzani wale ambao wamefungwa kisiasa na ni mahabusu wa siasa waachiliwe huru,” amesema

Amesema “ni aibu kwa nchi hii kumshikilia mtu ambaye baba yake alipambana, amelipa fedha kwa ajili ya kuipigania nchi hii, halafu aipindue nchi? Mtu ambaye baba yake hajaongoza mapambano ndiyo wanamtesa mtu ambaye baba yake alipigania nchi hii,” amesema Askofu Mwamakula.

“Tunatoa wito kwa Rais Samia kumuachia Mbowe, siingilii mahakama nisikilizeni waliopeleka mashtaka si serikali? wanaoweza kuondoa kesi ni wao, anaweza kutoa maelekezo kuondoa kesi mahakamani. Rais atoe maelekezo kwa DPP aliyemteua aondoe mashtaka yaliyopo mahakamni.”

Wakati huo huo, Askofu Mwamakula ameiomba Serikali iondoe zuio la mikutano ya vyama vya siasa.

“Tunatoa wito kwa serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia iachilie uhuru wa mikutano ya kisiasa ya hadhara, kuifungia ni kinyume cha katiba ni kufinya haki,” amesema Askofu Mwamakula.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!