Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe: Askari polisi adai haina maslahi binafsi
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe: Askari polisi adai haina maslahi binafsi

Spread the love

 

MKAGUZI wa Jeshi la Polisi Tanzania, Tumaini Swila, amedai kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, haijafunguliwa kwa sababu ya maslahi binafsi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Inspekta Swila anayedaiwa kuwa mpelelezi msaidizi wa kesi hiyo, ametoa kauli hiyo leo Jumanne, tarehe 7 Februari 2022, mahakamani hapo, akiulizwa maswali ya dodoso na Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi, Peter Kibatala, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni waliokuwa makomando wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Kibatala alimhoji Inspekta Swila, kama aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, hakuwa na maslahi katika kesi hiyo, kwa kuwa alikuwa mlalamikaji na msimamizi wa upelelezi wake, ambapo alijibu akidai hana maslahi.

Mahojiano kati ya Wakili Kibatala na Inspekta Swila kuhusu suala hilo yalikuwa kama ifuatavyo;

Kibatala: Nimekusikia ukisema kwamba DCI ndiye aliyepokea taarifa ya kwanza kutoka kwa Luteni Urio?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: DCI ni bosi wako wewe, ACP Ramadhan Kingai, Goodluck, Mahita, Jumanne Malangahe, Hassan Msangi, Ndowo na Madembwe, wote DCI ni bosi wenu?

Shahidi: Ni sahihi lakini kamisheni ni tofauti.

Kibatala: Bosi wenu DCI mwishoni IGP?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Ni sahihi bosi wenu alikuwa mlalamikaji wa kesi wanayoshtakiwa kina Mbowe?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Ni sahihi kwa ushahidi wako kwamba bosi wenu DCI tu-assume labda kama kweli, ndiye alipokea taarifa kutoka kwa Urio, akashusha maelekezo akamuita Kingai kumpa maalekezo?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Kuna msaidizi wa DCI?

Shahidi: Ndiyo yupo.

Kibatala: Anaitwa nani?

Shahidi: Alikuwa Charles Kenyera refer.

Kibatala: Unafahamu kwamba DCI angekuwa anacomply yeye kama mlalamikaji angetakiwa amwachie msimamizi wake ili kuondoa confirmation biased?

Shahidi: Sio kweli.

Kibatala: Katika utaratibu wa kawaida, RPC amekutuhumu kwa kosa fulani yule afande RPC anaruhusiwa kupeleleza kesi hiyo?

Shahidi: Ni tofauti na upelelezi wa jalada, unavyoongea, ni vitu viwili tofauti.

Kibatala: Swali langu ni kwamba, unakubaliama na mimi RPC haruhusiwi kwenye huo mchakato yeye atakuja kutoa ushahidi?

Shahidi: Kwa mazingira hayo ni sahihi.

Kibatala: Kwa nini RPC haruhusiwi?

Shahidi: Rudia.

Kibatala: Nimekuuliza RPC akikutuhumu wewe kwa tuhuma fulani anaruhusiwa kushughulikia hilo suala?

Shahidi: Si anawapa watu wa chini yake kufanya kazi

Kibatala: Logic yake ya kisheria ni nini?

Shahidi: Ni utaratibu wa kazi.

Kibatala: Uliwekwa kwa kuzuia nini, kitu gani walikuwa wanakiepuka pale?

Shahidi: Ni utaratibu wa kazi hakuna kitu chochote kinachokiukwa.

Kibatala:Order iliyotoka kwa DCI wewe unaweza kui-challenge?

Shahidi: Inategemea.

Kibatala: Na nini?

Shahidi: Order yenyewe.

Kibatala: DCI au Kingai akikwambia fungua jalada la tuhuma za ugaidi unaweza kumbishia?

Shahidi: Ndiyo nafungua.

Kibatala: Swali langu unaweza kumbishia?

Shahidi: Kama ni sahihi nitafungua.

Kibatala: Nasema hivi wewe ndiyo ulifungua faili la watu kula njama za kutenda vitu vya kigaidi, swali langu ulikuwa na materio gani ya kukuwezesha kufungua faili?

Shahidi: Uwepo wa taarifa hizo.

Kibatala: Hiyo taarifa ulipewa wewe?

Shahidi: Alipokea Afande Boaz

Kibatala: Mpaka muda huo ulikuwa bado hujaongea na Urio au ulikuwa umeshaongea naye?

Shahidi: Ilikuwa bado.

Kibatala: Kwa hiyo ulikuwa huna ufahamu wa moja kwa moja wa taarifa zingekuwezesha kufanya analysis ili ujue ufungue kesi gani?

Shahidi: Taarifa zilikuwepo.

Kibatala: Ulikuwa ushamhoji Afande Boaz kujua hiyo hear say kufanya assesment ya uchunguzi wako?

Shahidi: Tarehe 14 Julai yeye alikuwa amepokea hizo taarifa, ilikuwa sahihi kufungua.

Kibatala: Aliyepewa taarifa ni Boaz akamshusha kwa Kingai, akakupanga wewe. Wewe uliongea ane ana kwa ana akakusimulia, ulikuwa ushamhoji Afande Boaz kujua alichosimuliwa na Urio?

Shahidi: Si ndiyo maana nikafungua jalada.

Kibatala: Ulikuwa ushamhoji Boaz maelezo yake ili ujue alichosimuliwa na Urio ni nini?

Shahidi: Yaani ile kufungua taarifa tayari kuna maelezo yake.

Jaji Tiganga: Swali liko hivi, wakati unakwenda kufungua jalada ulishamhoji na kumuandika maelezo Boaz?

Shahidi: Ilikuwa bado.

Kibatala: Na tunakubaliana kwamba, wakati wanaongea, Urio mtoa taarifa na Boaz mlalmikaji, wewe hukuwepo, sahihi?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Bado unatusisitizia ulikuwa na material ya kutosha kufungua kesi yenye tuhuma za ugaidi?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Unafahamu maana ya hear say?

Shahidi: Taarifa za kusikia.

Kibatala: Na uzito wake kwenye ushahidi?

Shahidi: Nafahamu.

Kibatala: Ulichofanyia kazi ni hear say au sio hear say? Sababu hukuongea moja kwa moja na Urio, hukuwa na maelezo ya DCI Boaz, hukuwa umemhoji urio, ulichofanyia kazi wewe sio hear say?

Shahidi: Haizuii kufungua kesi.

Kibatala: Swali langu ni hear say, sio hear say?

Shahidi: Ni hear say lakini haizuii kufungua kesi.

Kibatala: Tujadili suala lingine, ni sahihi kwamba at the end of the day aliyekuwa anasimamia suala la upelelezi wa kesi hii iliyomfikisha Mbowe na wenzake kuwa mahakamani ni Boaz?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Ripoti zote mwisho wa siku aidha moja kwa moja au sio moja kwa moja, zilikuwa zinaenda kwake yeye?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Barua zote za uchunguzi zilikuwa zinatoka direct or indirect kwa Boaz?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Na huyu ambaye alikuwa anafanya hivyo, unaona kwamba hana maslahi binafsi kwenye hili suala?

Yeye ndiyo mlalamikaji, amepokea ripoti yeye, anasema fungua faili limefunguliwa kwa hear say, anaunda timu ya upelelezi, alikuwa na maslahi kwenye hilo suala?

Shahidi: Hana maslahi binafsi.

Kibatala: Unafahamu maana ya maslahi binafsi na viashiria vyake?

Shahidi: Ndiyo.

Kibatala: Na hapa huvioni?

Shahidi: Havipo.

Kibatala: Heshima binafsi ya DCI kama mpelelezi mkuu kwenye suala hili na uwezo wake wa kuelewa mambo ni moja wapo ya mambo yanayojadiliwa kwenye kesi hii au lah?

Shahidi: Rudia.

Kibatala: Nasema pride, intergrit ya DCI kama mpelelezi makini katika suala hili, linajadiliwa halijadiliwi?

Shahidi: Kinachojadiliwa na kesi kosa wanalofanya watuhumiwa, ndiyo kilichopo mahakamani tunachojadili.

Kibatala: Aliyepokea taarifa ni nani?

Shahidi: DCI mwenye jukumu la kusimamia upelelezi nchi nzima

Kibatala: Ndio maana na kuuliza kuna maslahi binafsi?

Shahidi: Hakuna maslahi binafsi.

Shahidi huyo wa 13 wa Jamhuri, anaendelea kutoa ushahidi wake mahakamani hapo mbele ya Jaji Tiganga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!