August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mattaka yakwama

Spread the love

KESI inayomkabili David Mattaka, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), iliyotajwa kusikilizwa leo, imeahirishwa, anaandika Faki Sosi.

Kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa Respicius Mwijage, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu imeahirishwa leo na hakimu Thomas Simba baada ya kutokuwepo kwa hakimu Mwijage.

Mshitakiwa huyo alipandishwa kizimbani Machi mwaka huu kwa kosa la kuiingizia serikali hasara ya Dola za Marekani 772,402.08.

Tuhuma hizo ni pamoja na kutia saini mkataba wa kukodisha ndege aina ya Air bus A320-214 kwa Kampuni ya Wallis TradingInc bila kufuata sheria na taratibu za zabuni, kuidhinisha pesa za matengenezo ya ndege hiyo kwa Kampuni ya AEROMANTENIMIENTO.

Hasara nyengine ni kununua vifaa vya ndani ya ndege hiyo vilivyoigharimu Dola za Marekani 35,984.82.

Watuhumiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Ramadhani Mlinga, Mkurugenzi wa Manunuzi ATCL na Bertha Soka ambaye ni mwanasheria wa shirika hilo. Watendaji hao wanadaiwa kushindwa kuzuia ubadhirifu huo. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 19 Machi.

error: Content is protected !!