Spread the love

 

MALALAMIKO dhidi ya Hakimu Mkazi wa Mahakama za Kinondoni na Kisutu, kugoma kufungua shauri la jinai dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, yametinga rasmi kwa Jaji Mfawidhi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na wakili wa mwasilisha maombi, Hekima Mwasipu, barua ya malalamiko iliyoandikwa na mwandishi wa habari, Saed Kubenea, kwenda kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, tayari ilipokewa juzi Jumatano.

Kubenea alifikia uamuzi huo, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, kugoma kuirejesha kesi hiyo ambayo tayari ilikuwa imefunguliwa mahakamani na kusajiliwa kama – Miscellaneous Criminal Application No. 7/2021.

Undani wa habari hii, soma Gazeti la Raia Mwema la leo Ijumaa 31 Desemba 2021, kujua kwa undani kilichotokea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *