Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya madai Dola 55 Mil dhidi ya Tanzania yafutwa Marekani
Habari za Siasa

Kesi ya madai Dola 55 Mil dhidi ya Tanzania yafutwa Marekani

Spread the love

KESI ya madai ya Dola za Marekani Milioni 55, iliyofunguliwa na Kampuni ya Transport Equipment Ltd (TEL) dhidi ya Serikali ya Tanzania nchini Marekani, imefutwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Familia ya Vipula Valambhia, mmiliki wa Kampuni ta TEL ambaye sasa ni marehemu, ilifungua madai hayo katika Mahakama ya Wilaya ya Columbia nchini Marekani.

Tarehe 31 Machi 2019 Mahakama ya Wilaya ya Colombia chini ya Jaji Tanya S. Chuktan, ilifuta kesi hiyo ya madai Na. 1:18-CV-370 (TSC) kutokana na mdai kukosa msingi ya kisheria na kwamba, hawakustahili kufungua kesi ya namna hiyo nchini Marekani.

Katika uamuzi wa kesi hiyo iliyofunguliwa tarehe 19 Februari 2018, mahakama hiyo ilieleza kwamba, madai yaliyowasilishwa na familia ya marehemu Valambhia hayakuhusisha shughuli za kibiashara zilizofanyika nchini Marekani kama ambavyo Sheria ya nchi hiyo ya Uniform Foreighn –Country Money Judgment Recognition Act inavyotaka.

Familia hiyo ilifungua kesi ya madai dhidi ya Tanzania ambapo walalamikiwa walikuwa ni Benki Kuu ya Tanzania (B.o.T) na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Msingi wa madai yao ni kuitaka mahakama hiyo kutambua na kutoa amri ya kukazia malipo ya fedha kiasi cha dola 55,099,171.66, zilizoamriwa na Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka 2003.

Katika madai hayo, walalamikaji walidai kwamba, kiasi hicho cha fedha kilipaswa kilipwe tangu tarehe 4 Juni 2001 pamoja na riba ya asilimia 7 kila mwaka, hivyo wakati wa kufungua shauri hilo tarehe 19 Februari 2018 deni halisi lilikuwa dola za marekani milioni 64.5.

Serikali ya Tanzania iliwasilisha utetezi wake kupinga shauri hilo tarehe 13 Julai 2018 ikisema kwamba, yalifunguliwa kinyume cha sheria ya taratibu za Sheria ya Marekani inayotambua na kuruhusu kukazia hukumu za kimahakama nchini Marekani.

Ilieleza kwamba, ina kinga ya kisheria kama nchi kufunguliwa madai ya kukazia hukumu za kimahakama nchini humo.

Upande wa walalamikaji walikiri kupitia maelezo yaliyowasilishwa mahakani hapo kuwa, shauri hilo linahusisha suala lilifanyika nje ya Marekani.

Msingi wa madai hayo ulitokana na Mkataba wa Ununuzi wa Vifaa vya Kijeshi kati ya Kampuni ya TEL na Serikali ya Tanzania ulioingiwa miaka ya 1980, kampuni hiyo ilidai kwamba, haijakamilishiwa malipo yote ya fedha zitokanazo na mkataba huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!