March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Luu yafika patamu Dar

Elizabeth Michael (Lulu) akitokea katika Mahakama Kuu

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepokea ushahidi wa mganga  wa tiba mbadala Josephine Mushumbusi aliyekuwa akimtibu Steven Kanumba matatizo ya moyo, anaandika Faki Sosi.

Maelezo ya ushahidi huo yalitolewa na askari aliyemrekodi  Mushumbusi aliyemhoji Aprili  23 Aprili 2012.

Mbele ya Jaji Sam Rumanyika wakili  Peter Kibatala aliiomba Mahakama  kupokea  ushahidi wa Sajenti  E103  Nyangea aliyerekodi maelezo ya Mushumbus ambaye hakufika mahakamani kutokana na kuwapo nje ya nchi.

Sajent Nyagea amesoma maelezo  aliyojiridhisha kuwa ndiyo aliyorekodi kama ushahidi.

Akisoma maelezo hayo ya Mushumbuzi aliyeeleza ambaye alisema kuwa Kanumba alifika kwenye kituo chake kinachoitwa Precious kilichopo Bunju Dar es Salaam mwezi Agosti mwaka 2011.

Alieeza kuwa  Kanumba alienda kwenye kituo hicho na kumfanyia vipimo vya mwili mzima na kubaini kuwa Kanumba ana matatizo ya moyo pamoja na kuwa na Rehemu mwilini  mwake.

Ameeleza kuwa Kanumba alibainika kuwa anafanya mazoezi ya kutanua misuli na kwamba alimshauri aache kwa sababu yangeweza kumsababishia matatizo ya kupooza au kufariki.

Shahidi huyo alieleza kwamba  Kanumba aliwahi kulalamika maumivu makali ya moyo.

Akisoma maelezo hayo Sajenti alieleza kuwa Mushumbusi alimshauri Kanumba arudi siku nyingene kwa kuwa siku hiyo muda  ulikuwa umeisha .Baada ya hapo Jaji Rumanyika aliahirisha kesi hiyo hadi kesho kwa ajili kusikiliza  maoni ya  wazee wa baraza.

error: Content is protected !!