Tuesday , 27 February 2024
ElimuHabari Mchanganyiko

Kesi ya Lusako bado

Alphonce Lusako, Mwanafunzi aliyefukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari wa MwanaHALISI Online
Spread the love

KESI ya Alphonce Lusako, mwanafunzi wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayehangaikia haki yake ya kikatiba ya kujiendeleza kielimu baada ya kunyimwa na chuo hicho, imekwama, anaandika Hellen Sisya.

Lusako amefungua kesi Mahakama Kuu kuomba kusikilizwa malalamiko yake ya kunyimwa fursa ya kusoma Shahada ya Sheria katika chuo hicho kwa sababu ambazo kwake hazina msingi hata kisheria.

Kesi hiyo ingali kwenye hatua ya kutafuta kibali cha mahakama hiyo kumruhusu kufungua malalamiko yake hayo. Leo ilikuwa ni siku ya kutolewa uamuzi mdogo wa maombi yake Na. 39 ya mwaka huu.

Hata hivyo, imelazimu uamuzi huo kuahirishwa mpaka Julai 31 kutokana na Jaji Pelagia Khaday kueleza kuwa anahitaji muda zaidi wa kupitia kesi hiyo.

Hatua hiyo imekuja wakati uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umeweka pingamizi kama njia ya kumzuia Lusako kufungua malalamiko yake rasmi ya kuonewa kuhusu dhamira yake ya kusoma katika chuo cha serikali na kwa mkopo unaotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB).

Msingi wa malalamiko ya Lusako hasa ni kuwa chuo hicho kimemfukuza kinyume cha kanuni na sheria za nchi.

“Ninakishtaki chuo kwa sababu sikutendewa haki. Kikatiba nina haki ya msingi ya kusoma. Lakini pia nina vigezo vya kusoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na nilikidhi vigezo vya kudahiliwa katika chuo hiki kwa ajili ya shahada ya sheria, baada ya kuidhinishwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU),” anasema.

Katika malalamiko yake anawakilishwa na wakili Edwin Enosy.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

Habari Mchanganyiko

Oryx wagawa mitungi 1000 kwa viongozi wa dini, wajasiriamali Moshi

Spread the loveVIONGOZI wa dini kutoka madhehebu mbalimbali pamoja na wajasiriamali katika...

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!