Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Lissu dhidi ya Ndugai, sasa yaiva
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Lissu dhidi ya Ndugai, sasa yaiva

Spread the love
MKAKATI wa Tundu Antipas Lissu, kumburuza mahakamani Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, kufuatia uamuzi wake wa “kumvua ubunge wa Singida Mashariki kiholela,” sasa umekamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea). 

Taarifa iliyotolewa kwa MwanaHALISI ONLINE na Lissu mwenyewe, leo Ijumaa, 19 Julai 2019, inaeleza kuwa taratibu zote za kufungua shauri hilo zimekamilika; na kesi kamili yaweza kufunguliwa muda wowote wiki ijayo.

“Kwa kiasi kikubwa, taratibu zote za kufungua kesi hii zimekamilika. Kilichobakia kwa sasa, ni kwa mawakili wangu kumalizia malizia kupitia nyaraka zote zinazohitajika, ili tukiende mahakamani tuende tukiwa tumejiandaa vya kutosha,” anaeeleza.

Lissu anasema,  aliamua kukaa kimya kwa muda mrefu kutokana na kujiandaa na suala hilo na kwamba hakutaka kwenda mahakamani bila kukamilisha kwa taratibu zinazotakiwa.

MwanaHALISI ONLINE liliripoti wiki hii, kwamba kesi ya Lissu dhidi ya Spika Ndugai, imekwama kufunguliwa mapema kufuatia kutokamilika kwa nyaraka muhimu, ikiwamo kukosekana kwa barua ya kumvua ubunge iliyoandikwa na Spika Ndugai kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Ndugai alitangaza kumvua ubunge Lissu, tarehe 28 Juni mwaka huu, kwa maelezo kuwa mwanasiasa huyo wa upinzani hafahamiki mahali aliko. Aidha, Ndugai alidai kuwa Lisuu amevuliwa ubunge kwa sababu ya kushindwa kuwasilisha kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa umma, taarifa za mali zake.

Kwa muda wa takribani miaka miwili sasa, Lissu yuko nje ya nchi kwa matibabu, kufuatia kushambuliwa kwa risasi na wanaoitwa na serikali, “watu wasiofahamika.”

Yafuatayo ni maelezo kamili ya Tundu Lissu, aliyoyatuma kwa MwanaHALISI na baadaye kusambazwa kwenye mitandao kadhaa ya  kijamii. 

Wakubwa salama?

Naona kuna watu wanahangaika sana na suala hili. Wapo ambao hawajawahi kututakia jema katika safari yetu ndefu ya kujenga demokrasia. Leo ndio wa kwanza kutoa machozi kwa kilichofanyika leo. Hayo ni machozi ya mamba na mimi sina haja ya kuwajibu. 

Kuna ambao wanalialia na kukata tamaa kwa sababu ya haya ya leo. Hawa nawaambia mapambano haya yanahitaji akili, sio jazba na hasira. Wengi hawaelewi kinachoendelea, wanafikiri haya ya leo ndio mwisho wa safari yetu. Hawa ndio ninahitaji kuwafafanulia kinachoendelea.

Kwanza, msichanganye ratiba ya Tume ya Uchaguzi na ratiba ya Mahakama Kuu. Ratiba ya Tume imekamilika leo. Wanachokiita uchaguzi kimefanyika. Kazi yao imekwisha. 

Ratiba ya Mahakama inaanza muda wowote kuanzia tarehe 29 Juni hadi 28 Desemba 2019. Maana yake ni kwamba ninaweza kufungua kesi katika siku yoyote ndani ya hicho kipindi cha miezi sita. 

Hadi sasa hazijafika wiki tatu tangu uamuzi wa Spika Ndugai. Bado nina miezi mitano na wiki moja ya kufungua kesi. Kwa hiyo wanaolialia kwamba nimeachia ngazi, etc., wajue sijachelewa hata kidogo. 

Pili, mwenye haki ya kufungua kesi hiyo ni mimi mwenyewe au mwakilishi wangu ambaye nimempatia mamlaka ya maandishi ya kushtaki kwa niaba, yaani power of attorney. 

Power of Attorney inatakiwa kusainiwa na mimi mwenyewe mbele ya kamishna wa viapo anayetambuliwa na sheria za Tanzania, basically wakili anayefanya kazi Tanzania anatakiwa kuja kunishuhudia sahihi huku niliko. 

Tatu, baada ya kusainiwa mbele ya kamishna wa viapo, power of attorney hiyo inatakiwa kusainiwa na huyo niliyemkabidhi mamlaka ya kuniwakilisha mahakamani, na saini yake hiyo ishuhudiwe pia na kamishna wa viapo. 

Nne, baada ya kusainiwa na wahusika wote, power of attorney hiyo inatakiwa kusajiliwa kwenye Ofisi ya Msajili wa Nyaraka Dodoma, Dar, Moshi au Mbeya na kulipiwa ushuru unaotakiwa. 

Tano, baada ya kusajiliwa ndio sasa kesi inaweza kufunguliwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.

Sita, sambamba na maandalizi ya power of attorney, nyaraka za kupeleka mahakamani zinatakiwa kuandaliwa kwa umakini mkubwa. 

Hakuna ruhusa ya kukosea kwenye maandalizi ya nyaraka hizi. Kosa moja dogo tu na kesi yote inatupiliwa mbali. Kesi ya Josh Nassari ni mfano mzuri. 

Saba, kwenye kesi hii sisi hatuna ugomvi wowote na Tume ya Uchaguzi. Mgomvi wetu ni Spika Ndugai na uamuzi wake. 

Tunachoenda kuiomba Mahakama Kuu iamue ni kama ni halali, kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanzania, kwa mbunge kuvuliwa ubunge kwa sababu zilizotolewa na Spika Ndugai, bila kuulizwa chochote au kupewa fursa ya kujitetea. 

Na, pili, tutaiomba Mahakama Kuu ijibu swali la kama kweli Spika Ndugai hakujua mahali niliko kwa muda wote huu tangu September 7, 2017. 

Mahakama Kuu ikikubaliana na Spika Ndugai, maana yake ni kwamba niliondolewa ubunge kihalali. Lakini ikisema kwamba Spika Ndugai alikuwa anajua niko wapi na alitakiwa anisikilize kwanza kabla ya kunivua ubunge, basi kilichofanyika leo kitakuwa sawa na sufuri. 

Nane, taratibu zote hizi za kufungua kesi zimekamilika kwa kiasi kikubwa. Kilichobakia ni kwa mawakili kumalizia malizia kupitia nyaraka zote ili twende mahakamani tukiwa na watertight case. 

Natumaini wiki ijayo haitaisha kabla hatujaenda Mahakama Kuu. 

Nimekaa kimya sana kwenye suala hili. Ukiwa maelfu ya kilometa nje ya nchi halafu unataka mambo yaende sawa Tanzania unahitaji utulivu na concentration. Vinginevyo utafanya makosa yanayotokana na upungufu wa umakini halafu utaonekana sio mtu makini. Natumaini maelezo haya yatakuwa yamewasaidia kupunguza hofu na kelele.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!