February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya kuvunja Muungano yakwama

Spread the love

MAHAKAMA ya Afrika Mashariki (EACJ) imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na wananchi ya kupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Uamuzi wa kesi hiyo iliyofunguliwa na Wanzanibar 40,000 wakiongozwa na Rashid Salum Adiy,  umetolewa jana tarehe 19 Septemba 2018 na mahakama ya EACJ.

Hata hivyo, jopo la majaji watano wakiongozwa na Jaji Kiongozi, Monica Mugenyi akiwa na majaji Fakihi Jundu na Dk. Charles Nyawelo waliokuwa wanasikiliza kesi hiyo, waliwashauri walalamikaji kuwasilisha madai yao katika mahakama za Zanzibar.

Katika kesi hiyo, wajibu maombi walikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo upande huo ulitetewa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi.

error: Content is protected !!