KESI ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Hashim Issa, imeahirishwa hadi tarehe 13 Desemba 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Imeahirishwa jana Jumanne, tarehe 23 Novemba 2021, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi, Rashid Chaungu kutokana na upande wa mashtaka kutokamilisha upelelezi.
Mwenyekiti huyo wa Baraza la Wazee Chadema, alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza tarehe 7 Oktoba 2021, ikiwa ni takribani wiki moja tangu alipofanya mkutano na waandishi wa habari, makao makuu ya chama hicho, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam.
Katika mkutano huo uliofanyika tarehe 1 Oktoba 2021, Issa anatuhumiwa kutoa tuhuma dhidi ya Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro.
Mzee Issa alisomewa mashtaka mawili ya uchochezi na Wakili wa Serikali, Yusuph Aboud, ambayo nikuchapisha taarifa ya uongo kwa njia ya kompyuta na kusambaza katika mtandao wa Youtube, kwa lengo la kumchafua na kumdhalilisha IGP Sirro.
Inadaiwa, Mzee Issa alimtuhumu IGP Sirro kuwa ni gaidi namba moja nchini Tanzania na fisadi, wakati si kweli.
Shitaka la pili ni uchochezi kinyme na kifungu cha 52(1) na 53(1) cha sheria ya huduma za vyombo vya habari kwamba “IGP Simon Sirro ni gaidi namba moja hapa nchini Tanzania ni fisadi.”
Asante sana kwa kutuhabarisha.
Japo kuna makosa machache ya maneno kama vile kinyme badala ya kinyume.
Uwe na maandalizi mema sana.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Real Estate Consultant