August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Kitilya , Sio, Sinare yaangukia Mahakama Kuu

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepokea jalada na kupanga tarehe ya uamuzi wa rufaa ya kesi inayowakabili Harry Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomon, anaandika Faki Sosi.

Kitiliya, alikuwa Kameshna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji na Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tawi la Tanzania.

Moses Mzuna, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam amesema kuwa, Mahakama Kuu itasikiliza rufaa ya upande wa mashtaka na kutoa uamuzi.

Jaji Mzuna amesema kuwa, upande wa utetezi bado utaweza kuleta hoja za uamuzi wa Mahakama ya Kisutu.

Jaji Mzuna amesema kuwa, mahakama hiyo itatoa uamuzi wa rufaa hiyo tarehe 7 Mei mwaka huu.

error: Content is protected !!