August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Kina Mdee: Chadema yaondoa mapingamizi, shauri kuanza kusikilizwa

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imekubali ombi la Wakili wa Chadema, Peter Kibatala, la kuondoa mapingamizi yao dhidi ya kesi ya Halima Mdee na wenzake 18 ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Mahakama umefanya uamuzi huo leo Jumatano tarehe 29, Juni, 2022 kufuatia maombi ya Kibatala ya kuondosha mapingamizi ya awali waliyowaweka kwenye Hati ya kiapo.

Kibatala ameiomba kuondosha mapingamizi hayo ili kupisha usikilizwaji wa shauri hilo kwa kuwa limefunguliwa mahakamani hapo kwa Hati ya dharura.

Jaji Mustapha Ismail amekubali ombi hilo na kuamua kuondoa mapingamizi hayo kabla ya shauri la msingi kuendelea kusikilizwa ambapo amesema kuwa amri ya zuio itaendelea mpaka shauri la msingi litakapofika mwisho.

“Baada ya kusikiliza hoja za Mawakili nimeamua Hati ya mapingamizi ya awali inaondolewa mapingamizi yote hayatataendelea”

Pia Jaji Mustapha amesema kuwa amri ya itaendelea mpaka mwisho wa shauri la msingi.
Wakati huo huo kolamu ya Mawakili imejitambulisha mbele ya Jaji kwa ajili ya kuendelea na shauri hilo.

error: Content is protected !!