Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya kina Mbatia, Selasini kuanza kusikilizwa kesho
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya kina Mbatia, Selasini kuanza kusikilizwa kesho

Joseph Selasini (kulia) na James Mbatia
Spread the love

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, kesho Jumanne, tarehe 24 Januari 2023, itaanza kusikiliza kesi Na. 570/2022, iliyofunguliwa na wajumbe wa zamani wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha NCCR-Mageuzi, kupinga uteuzi wa wajumbe wapya, wakidai ulikuwa kinyume cha sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kesi hiyo itasikilizwa mbele ya Jaji Ephery Kisanya, mahakamani hapo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, leo Jumatatu, tarehe 23 Januari 2023, Wakili wa upande wa waleta maombi, Hudson Mchau, amesema kesho mawakili wa pande zote mbili watawasilisha hoja mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa kisha Jaji Kisanya atapanga tarehe ya kutoa uamuzi.

Kesi hiyo ilifunguliwa mwishoni mwa 2022 na wajumbe wa zamani wa bodi ya wadhamini ya NCCR-Mageuzi, wanaodaiwa kuondolewa katika wadhifa huo, wakipinga wajumbe wapya kwa madai kuwa wameteuliwa kinyume cha sheria.

Kesi hiyo ilifunguliwa na wajumbe wa zamani akiwemo Mohamed Tibanyendera, Sam Ruhuza, Thomas Nguma dhidi ya wanaodaiwa kuwa wajumbe wapya wa bodi hiyo, wanaoongozwa na Makamu Mwenyekiti mpya wa NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini, akiwemo Esther Komba na wengine, Wakiiomba mahakama hiyo itamke wajumbe wapi halali.

Wajumbe hao wa zamani wanaoongozwa na Mbatia, walifungua kesi hiyo siku chache baada ya upande wa kina Selasini, kugonga mwamba katika kesi yao waliyofungua mahakamani hapo kuwapinga kwa madai kwamba si halali kwa kuwa wamefukuzwa ndani ya chama hicho.

Desemba 2022, mahakama hiyo mbele ya Jaji Kisanya, iliondoa mahakamani Kesi Na. 459/2022 iliyofunguliwa na wajumbe hao wapya wanaoongozwa na Selasini, kwa kuwa yalikuwa na dosari za kisheria kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kumshtaki mjumbe aliyefariki dunia.

Akifafanua zaidi kuhusu kesi hiyo, Wakili Mchau amedai endapo mahakama itaamua kwamba wajumbe wa zamani ni halali na waliondolewa katika nyadhifa zao kinyume cha sheria, kesi yao ya msingi Na. 150/2022 waliyofungua kupinga kufukuzwa NCCR-Mageuzi itaendelea ili upande wa wajibu maombi waeleze ni mchakato gani uliotumika kuwaondoa madarakani.

Amedai kuwa, kama mahakama itaamua kwamba wajumbe wa zamani waliondolewa kwa mujibu wa sheria na kwamba wajumbe wapya ndiyo halali, watakuwa na kazi ya kutetea hoja yao kwamba wamefukuzwa kinyume cha sheria

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

error: Content is protected !!