Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi ya kina Kitilya yatua Mahakama ya Mafisadi
Habari Mchanganyiko

Kesi ya kina Kitilya yatua Mahakama ya Mafisadi

Spread the love

SERIKALI imeiomba amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuhamisha kesi ya uhujumu uchumi aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitiyla na wenzake, kwenye Mahakama Kuu kitengo cha Ufisadi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni Shose Sinara Miss Tanzania mwaka 1996 pia  alikuwa Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Benki ya Stanbic na Sioi Solomon, Mwanasheria wa Stanbic Tanzania.

Wengine aliyekuwa Kamishna wa Sera na Madeni Wizara ya Fedha, Bedason Shallanda (kwa sasa yuko Ofisi ya Waziri Mkuu) na Alfred Misana, ambaye alikuwa Kamishna Msaidizi wa Serana Madeni kutoka wizara hiyo ambaye kwa sasa yuko wizara ya afya.

Leo Tarehe 12 Februari  2019 akiongoza jopo la mawakili wa serikali Wakili Mwandamizi, Fredrick Manyanda mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi amewasilia ombi hilo liloambatana mashahidi 54 akiwemo aliyekuwa Waziri wa Fedha awamu ya nne Mustafa Mkuro na wengine saba kutoka nje ya nchi.

Ameieleza mahakama kuwa kwenye ombi hilo kuna nyaraka za mawasiliano ya simu na barua pepe, nyaraka za benki, barua mbalimbali 218.

Upande wa mashatka umepanga kuanza kuita mashahidi hao  kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi hiyo kwenye mahakama ya ufisadi.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwenye Mahakama Kuu kitengo cha Ufisadi.

Kesi hiyo  namba  2 ya mwaka 2019, Kitilya na wenzake kwa pamoja wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 58, na mashtaka 49 ni ya utakatishaji fedha, mashtaka matatu ya kughushi na mawili ya kutoa nyaraka za uwongo.

Mashtaka mengine shtaka moja la kuongoza mtandao wa uhalifu, shtaka moja la kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu moja lingine la kula njama za kutenda kosa kwa nia ya kumdanganya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti tofauti kati ya Februari 2012 na Juni 2015 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na nje ya nchi.

Makosa hayo yalitokana na mchakato wa kuiwezesha Serikali kupata mkopo wa Dola za Marekeni 550 milioni kutoka Benki ya Standard ya Uingereza, kwa ada ya uwezeshaji ya asilimia 2.4, kupitia kampuni ya Egma Ltd.

Katika mashtaka hayo wanadaiwa kujipatia Dola za Marekani 6 milioni kwa njia za udanganyifu kupitia kampuni ya Enterprises Growth Market Advisors (EGMA) kama ada ya uwezeshaji wa mkopo huo ya asilimia 2.4 na kisha kutakatisha kiasi hicho cha fedha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!