Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Halima Mdee na Wenzake kuanza kusikilizwa kesho
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Halima Mdee na Wenzake kuanza kusikilizwa kesho

Spread the love

KESI ya waliokuwa wanachama na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18, ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho inatarajiwa kuanza kusikilizwa kesho. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Kesi hiyo namba 36 ya mwaka 2022 imepangwa kusikilizwa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji Cyprian Mkeha.

Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake walifungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu wakipinga uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema wa tarehe 11 Mei, 2022 kuwavua uanachama, kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review).

Walifungua kesi hiyo tarehe 21 Julai 2022 ikiwa ni siku ya 13 baada ya kupata ridhaa ya mahakama hiyo.

Akizungumza na MwanaHALISI online leo tarehe 28 Julai, 2022, Wakili anayewawakilisha Halima Mdee na wenzake Dickson Kilatu amesema kesi hiyo imeitishwa kesho kwa maelekezo ya Mahakama.

Wakili wa Chadema, wakiongozwa na Peter Kibatala (katikati) wakiwa mahakamani

“Kesi imepangwa kesho tarehe 29 Julai saa tano kwa ajili ya maelekezo ya mahakama kwenye shauri hilo” ameeleza Kilatu.

Katika kesi hiyo Mdee na wenzake wanaowakilishwa na mawakili Kilatu, Ipilinga Panya, Aliko Mwamanenge na Emmanuel Ukashi, wanaiomba mahakama hiyo ipitie mchakato na uamuzi huo wa Chadema kuwafukuza  kisha itoe amri tatu.

Amri hizo ni ya kutengua mchakato na uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama, kukilazimisha Chadema kutimiza wajibu wake kisheria, yaani kuwapa haki ya kusikiliza na amri ya zuio dhidi ya Spika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kutokuchukua hatua yoyote mpaka malalamiko yao yatakapoamuriwa.

Uamuzi huo wa Baraza Kuu ulitokana na rufaa walizozikata kina Mdee kupinga uamuzi wa awali wa kuwavua uanachama uliotolewa na Kamati Kuu, tarehe 27 Novemba, 2020, iliyowatia hatiani kwa kosa la kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum, bila ridhaa ya chama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!