August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Bob Wangwe yapigwa kalenda 

Spread the love

UPANDE wa Mashtaka umeshindwa kuwafikisha mashahidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni inayomkabili Bob Chacha Wangwe (24), kutokana na dharula ya kikazi, anaandika Faki Sosi.

Bob ni mtoto wa marehemu Chacha Wangwe, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, mkoani Mara na Makamu Mwenyekiti wa Chadema- Bara.

Paul Kadushi, wakili wa Serikali  mbele ya Huruma Shahidi, Hakimu Mkazi Mkuu,  amedai kuwa leo ilikuwa ni siku ya kupeleka mashahidi mahakamani hapo, hata hivyo kutokana na mashaihidi hao kuwa katika safari za kikazi akaiomba mahakama ihairishe kesi hiyo.

Katika kesi hiyo namba 167, Chacha Wange anatuhumiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.

Anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo tarehe 15 Machi na kwamba alichapisha taarifa iliyosema, “….Tanzania ni ambayo inajaza chuki wananchi.… matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya Muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania Bara kwasababu za kijinga.”

Kesi hiyo itatwajwa tena tarehe 13 Oktoba, mwaka huu ambapo inatarajiwa kuwa, upande wa Jamhuri utapeleka mashahidi wake.

error: Content is protected !!