July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ‘picha za ngono’ yakwama

Spread the love

WASHTAKIWA wanne wa kesi ya kusambaza picha za ngono za msichana wa miaka 21 wilayani Mvomero, Morogoro imekwama tena baada ya kukosa dhamana, anaandika Christina Haule.

Hatua hiyo inatokana na Ivan Msacky, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kusisitiza kukamilika kwa siku 60 alizotoa kwa waendesha mashtaka wa serikali kuwakilisha cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) juu ya zuio la dhamana hiyo.

Washtakiwa hao Rajab Salehe, Ramadhani Ally, Muksin Ng’ahy na John Peter licha ya mawakili wao Mohamed Mkali na Ignas Punge kuiomba mahakama leo kuwapa dhamana, bado wamegonga mwamba.

Hakimu Msacky amesema, licha ya kukamilika kwa upelelezi wa kipolisi juu ya shauri hilo na kufanya kesi hiyo kutaka kuanza kusikilizwa, bado anasimamia uamuzi wake wa kusubiri siku 60 ili kulinda usalama wa washtakiwa hao jambo ambalo litaelezwa zaidi na DPP.

Awali, washtakiwa hao wakiwa sita pamoja na wenzao wawili waliohusika na kesi hiyo Idd Adam Mabela na Zuberi Thabiti, walisomewa mashataka kwa hatua ya awali mahakamani hapo ambapo wote kwa pamoja walikiri kukamatwa na kushtakiwa huku wakikana kosa la kurekodi picha chafu na kusambaza.

Waendesha mashtaka wa serikali Grolia Rwakibalila, Edgar Bantulaki na Kalistus Kapinga wamesema mahakamani hapo kuwa, washtakiwa wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa kupiga picha chafu za ngono na kuzisambaza kwenye mtandao wa kijamii wa whatsapp kwa kutumia simu zao jambo ambalo ni kosa la jinai kwa sheria namba 54 ya mwaka 2016.

Hakimu Msacky ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 21 itakapoanza kusikilizwa.

Hata hivyo, waendesha mashtaka wa serikali wamelazimika kuahirisha kesi ya kubaka inayowakabili Idd Adam Mabela na Zuberi Thabit hadi julai 27 kufuatia hakimu aliyepaswa kuisikiliza, Mary Moyo kuwa likizo.

error: Content is protected !!