May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi mauaji ya Jamal Khashoggi yaanza tena

FILE - In this Jan. 29, 2011 file photo, Saudi journalist Jamal Khashoggi speaks on his cellphone at the World Economic Forum in Davos, Switzerland. Khashoggi was a Saudi insider. He rubbed shoulders with the Saudi royal family and supported its efforts to nudge the entrenched ultraconservative clerics to accept reforms. He was a close aide to the kingdom’s former spy chief and was a leading voice in the country’s prominent dailies. In a dramatic twist of fate, Khashoggi disappeared on Tuesday, Oct. 2, 2018, after visiting his country’s consulate in Istanbul and may have been killed there. (AP Photo/Virginia Mayo, File)

Spread the love

MAHAKAMA ya mjini Istanbul nchini Uturuki, imeanza vikao vya kusikiliza kesi inayohusu mauaji ya aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Saudi Arabia na mwandishi wa habari mahiri, Jamal Khashoggi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika kesi hiyo, watu 26 wanashitakiwa kwa mauji ya Khashoggi yaliyofanyika mwaka 2018, katika ubalozi wa Saudi Arabia, nchini Uturuki.

Mahakama mjini Istanbul inaendelea na shauri hilo, bila washitakiwa hao 26 kuwepo mahakamani. Serikali ya Saudi Arabia, imekataa kuwahamishia watuhumiwa hao Uturuki.

Miongoni mwa wanaotuhumiwa na mauaji ya Khashoggi, ni Ahmed al-Asiri, aliyekuwa naibu mkuu wa ujasusi, na Saud al-Qahtani, mshauri wa zamani wa mrithi wa kiti cha Ufalme, Mohamed Bin Salman.

Mwili wa mwandishi huyo wa habari wa gazeti la Washington Post la Marekani ambaye wakati mmoja alikuwa mtu wa karibu na familia ya Kifalme lakini akageuka kuwa mkosoaji mkubwa wa mwanamfalme, unaelezwa kuwa ulikatwa vipandevipande na kusafirishwa kwa mabegi maalum kurejeshwa Saudia.

Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi wa Saudia mjini Istanbul, tarehe 2 Oktoba 2018.

Alikwenda kwenye ubalozi huo, kufuatilia nyaraka za udhibitisho wa talaka aliyompa aliyekuwa mke wake, ili kumuwezesha kufunga ndoa na mchumba wake mwingine, Hatice Cengiz, raia wa Uturuki.

Cengiz alisema alimsubiri Khashoggi nje ya ubalozi huo kwa saa 11 lakini hakufanikiwa kumuona tena.

Alisema, Khashoggi alihitajika kusalimisha simu yake ambayo ni sheria kwenye balozi nyingi. Alimuambia ampigie simu mshauri wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ikiwa hangerudi kutoka ndani ya ubalozi huo.

Khashoggi, mwandishi maarufu wa habari ulimwenguni aliyeangazia taarifa kubwa kwa mashirika tofuati nchini Saudia.

Aliunda urafiki na Osama bin Laden katika miaka yake ya kwanza alipoanza kuwa mwandishi habari na alifahamika kama mzaliwa maarufu wa Saudia aliyelazimika kutoroka nchi hiyo.

Kabla ya kutoweka kwake katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul, uhamisho wa kibinfasi wa Khashoggi ulimlazimu kuishi baina ya Marekani, Uingereza na Uturuki.

Aliondoka Saudi Arabia mnamo Septemba 2017, baada ya kukosana na maafisa katika ufalme wa nchi hiyo.

Akiwa uhamishoni, alikuwa akiandikia gazeti la Washington Post Marekani nakala kali za kuukosoa utawala wa Saudia, na pia katika akunti yake ya Twitter ambako alikuwa na wafuasi zaidi ya 1.6 milioni.

Alisafiri mara kadhaa kwenda Afghanistan, kufanya mahojiano na Osama Bin Laden. Alifahamiana na Bin Laden tangu akiwa kijana nchini Saudi Arabia.

Wakati huo, Bin Laden alikuwa bado hajafahamika sana katika mataifa ya Magharibi kama kiongozi wa kundi la al-Qaeda.

Khashoggi alitembelea mapango ya Bin Laden yaliokuwa kwenye milima ya Tora Bora; na aliwahi kufanya mahoajino naye akiwa nchini Sudan mwaka 1995.

Alikuwa karibu na watawala wa Saudia, akikutana mara kwa mara na familia ya ufalme.

Alishikilia nyadhifa tofuati na alifanya kazi na vituo kadhaa vya TV akinza kama mwandishi wa masuala ya nje ya nchi, hadi kuwa mhariri mkuu.

Kituo cha Al-Arab kilionekana kuwa mpinzani kwa shirika la utangazaji la Al-Jazeera, linalofadhiliwa na Qatar.

Lakini muda mfupi baada ya kuzinduliwa, kituo hicho cha televisheni kilichokuwa chini ya usimamizi wa Khashoggi kilifungwa, kufuatia kurusha mahojiano na kiongozi wa upinzani wa Bahraini.

Khashoggi kwa wakati huo pia alikuwa akihojiwa na vyombo vya habari vya mataifa ya nje, akishutumu ufalme wa Saudi Arabia, akieleza kwamba kuna haja ya kuwa na mfumo wa kidemokrasia kuhakikisha utulivu wa nchi hiyo katika miaka ijayo.

Wakati maandamano ya machipuko katika nchi za kiarabu yalipoanza, kudai mabadiliko ya uongozi Khashoggi alikuunga mkono upinzani uliotaka mabadiliko nchini Misri na Tunisia.

Msimamo wake ulikuwa kinyume na sera rasmi ya ufalme wa Saudia, uliotazama maandamano hayo kama tishio kwa uwepo wake.

Mwandishi huyo wa zamani aliondoka Marekani mnamo Septemba 2017, akimshutumu kiongozi wa kudumu wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Mohammed bin Salman, kwa kulenga upinzani kwa “kujifanya kama Putin.”

“Nimeondoka nyumbani kwangu, nimeiacha familia yangu na kazi yangu na ninapaza sauti yangu,” alisema “kufanya jambo jingine lolote itakuwa ni kuwasaliti wanaoteseka gerezani. Naweza kuzungumza wakati wengi hawawezi.”

“Naweza kusema Mohammed bin Salman anajifanya kama Putin. anatenda haki ki ubaguzi,” aliandika katika nakala kwenye gazeti la Washington Post.

Aliendelea na shutuma zake dhidi ya kiongozi wa Saudia hadi alipoingia katika ubalozi huo mjini Istanbul na hiyo ikawa mwisho wa kuonekana kwake.

Kwa mujibu wa mashitaka ya Uturuki, Khashoggi alinyongwa hadi kufa na mwili wake kukatwakatwa vipande. Mabaki yake, hayakuwahi kupatikana.

error: Content is protected !!