Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi kupinga wakurugenzi kusimamia chaguzi; serikali yakwama kortini
Habari Mchanganyiko

Kesi kupinga wakurugenzi kusimamia chaguzi; serikali yakwama kortini

Mahakama Kuu ya Tanzania
Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi la serikali kwenye shauri la kupinga utaratibu wa kuteuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri kuwa wasimamaizi wa uchaguzi. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Kesi hiyo iliyofunguliwa na  Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe ambapo leo tarehe 13 Februari 2019, mahakama imeelezea kuwa, waombaji wanahaki ya kisheria kufungua shauri hilo.

Awali serikali ilitaka kesi hiyo itupiliwe mbali kwa sababu, waombaji hawakustahili kufika mahakamani na badala yake kwenda kulalamika kwenye utawala wa tume.

Tarehe ya kuendelea kusikilizwa kesi hiyo itatajwa saa nane mchana baada ya mahakama kurejea tena.

Bob Chacha Wange kupitia wakiliwa wake Fatma Karume amemshtaki Mwanasheria  Mkuu wa Serikali (AG), Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC)  na mkurugenzi  wake.

Bob Chacha Wangwe amefungua kesi hiyo kikatiba baada ya kuamini kuwepo kwa udhaifu wa tume hiyo. Amedai kuwa, tume hiyo inaongozwa na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao hawaendishi uchaguzi wa haki.

Bob Chacha Wange ni mtoto wa marehemu Chacha Wangwe aliyewahi kuwa Mbunghe wa Tarime mjini (Chadema).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!