December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi kupinga matokeo ya urais: Tanzania yapewa siku 45 kujitetea  

Nyundo ya Hakimu

Spread the love

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepewa siku 45 na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu  (ACHPR) kupeleka majibu yake katika kesi iliyofunguliwa na Wakili Msomi, Jebra Kambole ya kupinga matokeo ya urais kutopingwa mahakamani. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa  tarehe 14 Februari 2019 na ACHPR na kusainiwa na Msajili wa mahakama hiyo, Dk. Robert Eno, zikipita siku 45 pasipo serikali kuepeleka majibu yake, Mahakama itaendelea na usikilizaji wa kesi hiyo.

Wakili Kambole aliifungua Kesi hiyo Na. 018/2018 mwaka jana dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiitaka Mahakama ya Afrika ipitie ibara ya 41 (7) ya katiba ya nchi ambayo imenyima mamlaka mahakama yoyote ile,  kuchunguza matokeo ya urais yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Katika hoja zake, Wakili Kambole anadai kuwa, ibara hiyo inakiuka Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu.

error: Content is protected !!