August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ‘Kifaru cha Jeshi’ yapigwa kalenda

Spread the love

UPELELEZI wa kesi inayowakabili Musa Mkama, Mhariri wa Gazeti la Dira na Prince Newton, mwandishi wa gazeti hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeahirishwa, anaandika Faki Sosi.

Wanahabari hao wanatuhumiwa kuandika habari za uongo na kudaiwa kuzua mtafaruku kwa jamii. Habari hiyo ilipewa kichwa cha habari ‘Kifaru cha kivita cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), chaibwa.’

Easter Martn, wakili wa serikali amedai kuwa, upelelezi wa kesi haujakamili hivyo ameimba mahakama kuahirisha shuri hilo.

Hakimu Respicius Mwijage, amehairisha kesi hiyo hadi tarehe 10 Julai Mwaka huu.

Watuhumiwa wa kesi hiyo wanadaiwa kutenda kosa hilo 20 Juni mwaka huu katika eneo la Kinondoni Biafra, jijini Dar es Salaam.

Na kwamba, washtakiwa hao waliandika na kuchapisha habari za uongo katika gazeti hilo toleo namba 424 la tarehe 20 hadi 26.

error: Content is protected !!