Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi dhamana ya Wakili Madeleka: Mahakama yaipa Serikali siku tatu
Habari Mchanganyiko

Kesi dhamana ya Wakili Madeleka: Mahakama yaipa Serikali siku tatu

Peter Madeleka, Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeipa Serikali siku tatu kuwasilisha kiapo kinzani katika kesi iliyofunguliwa na watetezi wa haki za binadamu kuomba dhamana ya Wakili Peter Madeleka, anayedaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu, tarehe 25 Aprili 2022 na Wakili wa Mdeleka, Jebra Kambole, muda mfupi baada ya kesi hiyo Na. 16/2022, kusikiliwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi. Upande wa Serikali uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga.

Wakili Jebra amedai, mahakama hiyo imepanga siku hizo, baada ya kukataa ombi la upande wa Serikali la kupewa siku 14 kwa ajili ya kuwasilisha kiapo kinzani.

“Serikali waliomba siku 14 kuleta kiapo kinzani lakini mahakama ikasema wiki mbili ni nyingi sana, Mahakama imeamua kuja kusikiliza kesi Ijumaa. Serikali imeambiwa hadi Alhamisi walete kiapo kinzani,” amedai Wakili Jebra.

Aidha, Wakili Jebra amedai, mahakama hiyo imeshindwa kutoa amri ya Madeleka kufikishwa mahakamani hapo kwa kuwa haina taarifa rasmi mahali aliko wakili huyo.

“Sababu hatuna uthibitisho kutoka kwa Serikali iwapo yuko mikononi mwao au hayuko mikononi mwao na yuko kwenye chombo gani, hadi sasa taarifa mabayo iko mahakamani haijulikani yuko sehemu gani. Ndiyo maana mahakama imeshindwa kutoa amri siku ya Ijumaa kuletwa mahakamani,” amedai Wakili Jebra na kuongeza:

“Tunategemea Ijumaa tutajua kama wanaye au hawana na kama atapata dhamana au hatapata dhamana.”

Kesi hiyo ilifunguliwa Ijumaa iliyopita na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), ikishirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), baada ya Madeleka kukamatwa tarehe 20 Aprili mwaka huu, akiwa maeneo ya Serena Hoteli, jijini Dar es Salaam.

THRDC na LHRC wamefungua kesi hiyo baada ya Madeleka kunyimwa dhamana, ambapo kwa mujibu wa Wakili wa THRDC, Paul Kisabo, wakili huyo anashikilishwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!