JUMUIYA ya Afrika Mashariki imesema Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na Rais wa Rwanda Paul Kagame wamekubaliana juu ya haja ya waasi wa M23 kusitisha mapigano na kujiondoa katika maeneo ya mashariki mwa Kongo.
Taarifa ya Jumuiya hiyo imeongeza kuwa Kagame amekubali pia kumsaidia Kenyatta kuwahimiza waasi wa M23 kutekeleza matakwa hayo.
Mbinu za kufanikisha hatua hiyo zitajadiliwa wakati wa duru ya pili ya mazungumzo katika mji mkuu wa Angola Luanda wiki ijayo.
Naibu msemaji wa Rais wa Kongo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa hatua hii inatia moyo kuona Paul Kagame ametambua kuwa anaweza kuwashawishi M23, lakini amesema wanasubiri kuona kitakachotokea katika uwanja wa vita.
Makabiliano ya hivi karibuni kati ya waasi wa M23 na vikosi vya Kongo yamepelekea maelfu ya watu kuyahama makazi yao.
Leave a comment