August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kenyatta awalilia walinzi wake

Baadhi ya magari yaliyoteketea kwa moto baada ya ajali iliyohusishwa na lori la gesi Neivasha, Kenya

Spread the love

UHURU Kenyatta, Rais wa Kenya ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za watu 40 zizopoteza ndugu zao katika ajari ya Lori la mafuta iliyotokea eneo la Naivasha, ambapo miongoni mwa watu hao wamo 11 waliokuwa walinzi wake, anaandika Wolfram Mwalongo.

Walinzi wa Rais Kenyatta walipata mkasa huo wakitokea Kaunti ya Bomet Magharibi mwa Kenya ambako walienda kuimarisha ulinzi kwa kiongozi huyo katika ziara na mikutano yake ya hadhara.

Manoa Esipisu, msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo amesema, “Tumepoteza maafisa 11 wa GSU ambao ni walinzi wa rais Uhuru Kenyatta wakati wakirejea jijini Nairobi.”

Maofisa hao walikuwa kwenye gari aina ya Land Cruiser yenye namba GK B 961G ambayo ililipuka katika ajali hiyo.

Tukio hilo lilotokea Disemba 11 mwaka huu katika eneo la Karai barabara ya Naivasha. Kwa mujibu wa Isaac Masinde, Kamanda wa Polisi Kaunti ya Nakuru, lori hilo la mafuta liligonga tuta na kupoteza mweleko hali iliyopelekea kugonga magari mengine 13 huku mlipuko ukitokea.

Masinde amethibitisha vifo vya watu 33 huku wengine wawili wakiendelea kupata matibabu katika hospitali ya Nairobi ambapo mtu mmoja yupo chini ya uangalizi maalumu (ICU) na mwingine anaendelea vizuri.

Joseph Nkaisery, Waziri wa Usalama wa Ndani amesema, uchunguzi unaendelea zaidi kuhusiana na tukio hilo lakini amewataka madereva kuwa makini katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu.

“Nawaomba Wakenya wawe watulivu, baada ya uchunguzi kubainika, watapewa ripoti kamili, madereva na watumiaji wengine wa barabara wawe makini katika kipindi hiki cha sikukuu.”

error: Content is protected !!