July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kenyatta asimamisha vigogo wa ufisadi

Rais Uhuru Kenyatta

Spread the love

RAIS Uhuru Kenyatta, amewasimamisha kazi wakuu wawili wa Shirika linalopambana na ufisadi nchini humo, siku moja tu baada ya Bunge kupitisha muswada unaowalaumu kwa uzembe na utepetevu.

Kwa mjibu wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC), lililokariri taarifa kutoka kwa msemaji wa Ikulu ya Rais Manoah Esipisu, Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, itaendelea na kazi yake licha ya kusimamishwa kwa wakuu hao wawili.

Wakuu hao ambao ni Mwenyekiti, Mumo Matemu na naibu wake, Irene Keino ambapo uchunguzi dhidi yao umeanza kuhusiana na tuhuma za kuzembea kazini na kutumia vibaya mamlaka yao.

Tangazo hilo limefanyika chini ya mwezi mmoja baada ya ripoti kutoka kwa tume hiyo kuwasilishwa kwa Rais Kenyatta, iliyosababisha kusimamishwa kazi kwa mawaziri wanne wa serikali na maafisa wengine 12, huku uchunguzi dhidi yao ukianzishwa.

error: Content is protected !!