MAOFISA wakuu wa Baraza la Mitihani nchini Kenya wamefutwa kazi kwa madai ya vitendo vya udanganyifu uliofanywa wakati wa mitihani ya kitaifa mwaka jana.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limeripoti kuwa, waliofukuzwa kazi ni Joseph Kivilu, Ofisa Mkuu Mtendaji wa Baraza hilo na Kibiru Kinyanjui, Mwenyekiti wa Bodi inayosimamia baraza hilo.
Kufutwa kwa wakuu hao kumekuja kufuatia tangazo lililotolewa kwenye kikao cha Meja Jenerari Joseph Nkaissery, Waziri wa Usalama na Masuala ya Ndani na Fred Matiang’i, Waziri wa Elimu mbele ya wanahabari.
Nkaissery amesema, hatua zitachukuliwa dhidi ya waliohusika katika udanganyifu huo na kuwa mwaka jana watahiniwa waliopatikana na makosa ya udanganyifu Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2015 waliongezeka kwa asilimia 70.
Hata hivyo, Prof George Magoha, aliyekuwa Naibu Kansela wa Chuo Kikuu cha Nairobi ameteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa bodi hiyo.
More Stories
Kikwete: Asiyekubali matokeo Uchaguzi Kenya aende mahakamani
Prof. Wajackoyah afanikiwa kupiga kura baada ya kusubirishwa kwa saa tatu
Kenyatta aisifu IEBC: Uchaguzi unaenda vizuri