April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kenya yaongoza kwa bajeti kubwa Afrika Mashariki

Spread the love

MATAIFA matano ya Afrika Mashariki jana tarehe 13 Juni 2019, yalitazamiwa kusoma bajeti zao kwa Mwaka wa Fedha 2019/20. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mataifa hayo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini. Hata hivyo, Sudani Kusini haikufanikiwa kuwasilisha bajeti yake kutokana na kutetereka kwa mausala ya usalama.

Katika bajeti hizo, Tanzania yenye idadi ya watu takribani 55,000,000 imepanga kutumia jumla ya Dola za Marekani 14.3 Bilioni.

Dk. Philip Mpango akiwasilisha mapendekezo ya bajeti hiyo amesema, sehemu kubwa ya makadirio hayo yatatumika katika kuimarisha miundombinu ya reli, barabara na umeme katika maeneo ya vijijini.

Wakati Tanzania ikipanga kutumia kiasi hicho cha fedha, Serikali ya Uganda yenye idadi ya watu 45,710,000 imepanga kutumia Dola za Marekani Sh. 9.1 bilioni.

Serikali ya Uganda imekumbana na ukinzani kutoka kwa wasomi na kada mbalimbali nchini humo kwamba, pamoja na mpango wa matumizi hayo, madeni ya nchini ni makubwa.

Hata hivyo, Matius Kassaja, waziri wa fedha wa Uganda amesema kuwa, bajeti hiyo imejikita zaidi kwenye ujenzi wa viwanda ikiwa ni pamoja na kuongeza utajiri na na ustawi wa waganda wote.

Serikali ya Kigali, Rwanda imepanga kutumia jumla ya Dola za Marekani 3.2 Bilioni ili kuimarisha uchumi wake ikiwa ni pamoja na maisha ya Wanyarwanda wote.

Burundi inayotajwa kuwa na idadi ya watu milioni 10.8, kwenye bajetiti yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 ikipanga kutumia Dola za Marekani 824 Milioni.

Wananchi wa Rwanda yenye makadirio ya watu 12,501,156, kwenye bajeti hii wameelekeza matarajio yake katika ajira kwa vijana, kuimarisha uwekezaji na viwanda. Pia kuimarisha miundombinu ya maji, barabara na umeme.

Katika bajeti yake, Taifa la Kenya lenye makisio ya watu 50,950,879 kwa mujibu wa taarifa yam waka 2018, limepanga kutumia kiasi cha Dola za Marekani 29.2 Bilion, kiasi hicho cha pesa ni kikubwa kuliko jumla ya bajeti ya nchi tatu (Tanzania, Uganda na Rwanda).

Akiwasilisha bajeti hiyo, Waziri wa Fedha nchini Kenya, Henry Rotich amesema kuwa bajeti hiyo imezingatia ndoto na azimio la Rais Uhuru Kenyatta la kuwekeza katika sekta nne ambazo ni Afya, Kilimo, Makazi na Uzalishaji viwandani.

error: Content is protected !!