May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kenya yaichapa Stars 2-1

Spread the love

 

TIMU ya soka ya Kenya ‘Harambee Stars’ imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars.’ Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mchezo huo, umepigwa leo Jumanne, tarehe 15 Machi 2021, Uwanja wa Nyayo na mchezo wa pili wa kirafiki utachezwa Alhamisi hii 18 Machi 2021, Uwanja wa Kasarani, kuanzia saa 1:00 usiku nchini humo.

Magoli hayo ya Harambee Stars, yamefungwa na Eric Kapaito dakika ya 20 na Abdalla Hassan dakika ya 58 huku goli la kufutia machozi la Taifa Stars, likitupiwa kimiani na Ayubu Lyanda dakika ya 38.

Stars iko Kenya kwa michezo hiyo ya kirafiki ili kujiandaa kwa michezo ya kufuzu michuano ya mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Equatorial Guinea na Libya.

error: Content is protected !!