September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kenya Airway yapata hasara ya mabilioni

Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya

Spread the love

SHIRIKA la Ndege la Kenya limetangaza kupata hasara ya kiasi cha Shilingi za Kenya 7. 59 Bil (Takriban 151 Bil za Tanzania ) kwa mwaka wa 2018. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa ya hasara hiyo ilitolewa tarehe 29 Aprili 2019 na jarida maarufu nchini Kenya la masuala ya uchumi na fedha la Business Daily kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter. 

Shirika la Ndege la Kenya limesema, hasara hiyo imetokana na ukubwa wa gharama za uendeshaji ikiwemo kupanda kwa bei ya mafuta na mishahara ya watumishi wa shirika hilo.

Aidha, hasara hiyo ni pungufu ukilinganisha na hasara iliyopata Shirika la Ndege la Kenya kwa mwaka wa fedha wa 2017 ambapo ilikuwa Ksh. 9.44 Bil.

Hata hivyo, shirika hilo limetangaza ongezeko la mapato ya kiasi cha Ksh. 114.45 bilioni ikilinganishwa na mwaka 2017 ambapo yalikuwa ni Ksh. 106.2 bilioni.

error: Content is protected !!