LENGAI Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro na wenzake watano, wamefikishwa katika Mahakama mkoani Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Sabaya na wenzake watano, wamefikishwa tena mahakama leo Ijumaa, tarehe 18 Juni 2021.
Ni baada ya kufikishwa kwa mara ya kwanza, tarehe 4 Juni 2021 na kusomewa mashtaka sita kwa mahakimu wawili tofauti.
Mara baada ya gari la magereza kuwasili mahakamani hapo, umati wa watu walikuwa wamejitokeza kushuhudia kinachoendelea.
Wenzake watano ni; Sylivesta Nyegu, Wadson Stanley, Enock Togolan, John Odemba na Daniel Mbura.
Sabaya na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka ya; unyang’anyi kwa kutumia silaha, kushiriki vitendo vya rushwa , kutakatisha fedha, uhujumu uchumi na kuongoza magenge ya uhalifu.
Kelele za baadhi ya wananchi waliokuwepo mahakamani zilisikika huku wengine wakisema ‘mwizi, mwizi, mwizi’
Tofauti na walivyofikishwa mara ya kwanza, leo Ijumaa, Sabaya alikuwa kavalia kaunda suti huku akiwa ameshikilia kitabu mkononi.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI na MwanaHALISI TV kwa habari na taarifa mbalimbali ya kitakachojili mahakamani
Leave a comment