October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

KCMC yapiga ‘stop’ wanufaika wa Bima ya Afya

Hospitali ya KCMC

Spread the love

HOSPITALI ya Rufaa ya KCMC imesitisha kutoa huduma za afya kwa wanufaika wa mashirika takribani saba kutokana na kudaiwa madeni yenye thamani ya Sh. 2.2 Bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 21 Januari 2019 na kitengo cha utawala cha KCMC, imetaja mashirika hayo ikiwemo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kampuni za bima ya afya za NSSF na AAR.

Akizungumzia kuhusu taarifa hiyo, Gabriel Chiseo, Afisa Habari wa KCMC amesema taasisi hizo zimekiuka makubaliano ya mkataba waliongia na hospitali hiyo, kwa kushindwa kulipa gharama zinazopaswa kulipwa kila mwezi.

Chiseo ameeleza kuwa, mashirika hayo yana madai tangu mwaka 2016 na kwamba kwa mujibu wa mkataba, yalitakiwa kulipa kila mwezi baada ya wanufaika wao kupewa huduma.

Amesema madeni hayo yanaipa mzigo KCMC kutokana na hospitali hiyo kuwa na jukumu la kutibu Watazania wasio kuwa na uwezo, na kuwataka walengwa kuwasiliana na mashirika yao ili kupewa namna ya kupata huduma ya afya baada ya hospitali hiyo kuisitisha.

error: Content is protected !!