Wapinzani wa Simba kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika klabu ya Kazier Chiefs wamewasili jana kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julis Nyerere na ndege binafsi aina ya FlySafari FA555 wakitokea nchini Afrika Kusini. Anaandika Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 10 jioni, ambapo kwenye mchezo wa kwanza Simba walipoteza kwa mabao 4-0.
Kaizer Chiefs wametua Dar es Salaam na kikosi cha wachezaji 23 pamoja na benchi la ufundi na viongozi tayari kwa mchezo huo.
Wengine ambao ni walinda mlango Bruce Bvuma na Daniel Akpey, kwa upande wa mabeki kuna Njabulo Blom, Reeve Frosler, Daniel Cardoso, Anthony Akumu Agay, Happy Mashiane, Mulomowandau Mathoho, Ramahlwe Mphahlele, Kgotso Moleko, Yagan Sasman, Siphosakhe Ntiya- Ntiya na Siyabonga Ngezana.
Kwa upande wa viungo ni Philani Zulu, Kearyn Baccus, Lebogang Manyama, Willard Katsande na Nkosingiphile Ngcobo huku washambuliaji wakiwa ni Bernard Parker, Samir Nurković, Leonardo Castro na Lazalous Kambole.
Leave a comment