June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kazi 959 za waandishi kuchuana MCT

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga

Spread the love

JUMLA ya kazi 959 zimepokelewa na Balaza la Habari Tanzania (MCT) kwa ajili ya kushindanishwa  katika makundi 21 ya Tunzo ya Umahili wa uandishi wa habari Tanzania (EJAT) mwaka 2014. Anaandika  Sarafina Lidwino … (endelea).Katibu

Kazi za mwaka huu zimeongezeka kutoka zile za mwaka 2013 ambapo kulikuwa na jumla ya kazi za kushindaniwa 907.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukanjanga amesema, kati ya kazi hizo 959 zilizowasilishwa , waandishi wa mkoa wa Dar es salaam wanaongoza kwa kuwasilisha kazi 412, Mwanza 198, Kagera 66, Zanzibar 46 na Arusha 37.

Mukanjanga amesema, kazi hizo zimewasilishwa na vyombo mbalimbali vya habari 69. Ametaja vyombo vilivyopeleka kazi nyingi kuwa ni The Guardian 137, Mwananchi 87, Afya Radio 68, RFA 63, SAUT FM 50, TBC 46 na TSN 42.

Ameeleza, “ jumla ya waandishi walio peleka kazi ni 392, wanawake wakiwa 119 na wanaume 273. Dar es Salaam wamejitokeza wengi kwa sababu vyombo vingi vya habari vipo huku”.

Hata hivyo amesema, makundi ya kushindaniwa yameongezeka, ni tofauti na walipoanza mwaka 2009 ambapo makundi yalikuwa 21. Hivi sasa kuna makundi mawili yameongezwa ambayo ni Gesi, Mafuta na uchimbaji wa madini.

Kwa mujibu wa Mukajanga, Jopo la majaji wa tunzo hizo wameshaapishwa kwa ajili ya kuanza kazi hiyo, wataongozwa na mwandishi mzoefu na mkufunzi wa uandishi wa habari, akiwa kama mwenyekiti , Chrysostom Rweyemamu.

Washindi wa EJAT 2014 na wa Tuzo ya Mafanikio katika maisha ya uandishi wa habari watakabidhiwa tuzo zao katika tamasha la usiku wa Aprili 24, 2015, itakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.

error: Content is protected !!