February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kauli yake dhidi ya Magufuli, Mdee kupanda Kisutu tena

Spread the love

HALIMA Mdee, Mbunge wa Kawe, jijini Dar es Salaam leo anapanda tena kizimbani kuendelea na shauri lake kuhusu kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli alilofunguliwa mwaka 2017. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Shauri hilo lipo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo tayari upande wa mashataka umetoa ushahidi wake akiwemo Mkuu wa Kituo cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga.

Katika shauri hilo Mdee akiwa katika Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) tarehe 3 Julai 2017 anadaiwa kutamka maneno machafu dhidi ya Rais Magufuli.

Mdee anaiwa kutamka “anaongea hovyohovyo, anatakiwa afungwe breki” ambapo kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo tarehe 10 Julai 2017.

Mahakama ya Kisutu leo Alhamis 7 Februari 2019 itaendele kusikiliza ushahidi kwenye kesi hiyo.

error: Content is protected !!