March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kauli ya Lissu siku 20 zilizopita kabla ya kupigwa risasi

Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Spread the love

TUNDU Lissu Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), kabla ya kupigwa risasi leo alitoa tahadhari kwamba anafuatiliwa na watu aliodai kwamba wanatoka usalama wa taifa.

Alitoa madai hayo Agost 18 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Lissu alionyesha hofu hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa hoteli ya Protea Tarehe 18 Agosti mwaka huu.

Lissu alidai kuwa anafutiliwa na watu hao kila mahala anapoenda. “Mimi naomba kabla sijaanza mazungumzo yangu nimuombe mkuu wa idara ya usalama wa Tiafa anaitwa Dk Modestus Kipilimba au Inspkta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro wale vijana ambao wamewatuma na kwa wiki tatu mfufulilizo wananifuata kila nilipo wanaotembea na gari aina ya Toyota Primire namba T 460 CQV jana niliwakaba kanisa St. Peter”

“Wakubwa hawa wa vyombo vyetu vya usalama wawaelekeze watumishi wao watumie muda na rasilimali za nchi hii wafanye kazi ya kupambana na wahalifu siyo kupoteza muda wao na pesa zetu kuhangaika na raia wanaoiwajibisha Serikali iliyo madarakani.”

“Kwa hiyo afande Sirro na afande Kipilimba fanyeni kazi ya kupambana na wahalifu tuachieni kazi ya kuwawajibisha walikuwepo madarakani kwa mujibu wa sheria.” Alisema Lissu.

error: Content is protected !!