August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kauli tano za Zitto, akiuelezea utawala wa Magufuli

Spread the love

ZITTO Zuberi Kabwe, Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, alipozungumza na wanahabari jana, makao makuu ya chama hicho Kijitonyama jijini Dar es Salaam, alionyeshwa kukerwa sana na utawala wa awamu ya Tano, chini ya Rais John Magufuli, anaandika Charles William.

Katika kuelezea hali ya sasa ya nchi, kiuchumi na kisiasa wakati akisoma tamko la Kamati Kuu ya ACT Wazalendo na wakati wa kujibu maswali ya wandishi wa habari, Zitto alitoa kauli tano nzito dhidi ya Rais Magufuli. Kauli hizo ni hizi;

  1. “Uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuitelekeza serikali yake kwa mtu mmoja, anayejifanya anajua kila kitu na anayejigeuza kuwa mshauri wa washauri wake kiuchumi, utaliangamiza taifa hili.”
  2. “Kwa sasa watanzania tunaye rais asiyejua kuchagua maneno ya kuzungumza, hajui azungumze nini, wapi na katika mazingira gani.”
  3. “Utawala wa Rais Magufuli tangu kuingia kwake madarakani, unafanya juhudi kubwa za kuchokonoa na kumomonyoa mshikamano na upendo tulio nao kama taifa kwa kutoa hotuba zinazochochea chuki na migawanyiko baina ya wananchi.”
  4. “Kila baya likifanywa na Rais Magufuli, chama chake kinakaa kimya. Inasikitisha sana chama kilichoasisiwa na baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere kinamruhusu Rais na mwenyekiti wake kuhubiri na kuchochea chuki baina ya wananchi huku akipuuza utawala wa sheria na Katiba.”
  5. “Mtu yoyote anayeamini kuwa, anaweza kupambana na rushwa au ufisadi huku akikanyaga na kupuuza sheria na katiba ya nchi, mtu huyo ni muongo, mtu huyo ni fisadi na kwa kweli yafaa adharauliwe na akataliwe.”
error: Content is protected !!