Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kauli 11 mwiba mkali kwa wapinzani kwa sasa
Habari za Siasa

Kauli 11 mwiba mkali kwa wapinzani kwa sasa

Huphrey Polepole, Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM (katikati) akiwa na wanachama wapya wa chama hicho
Spread the love

VYAMA vya upinzani leo vimepata pigo baada ya kuondokewa na wanachama wake na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM), lakini mbali na pigo hilo maneno yaliyosemwa na wanachama hao ni mwiba mkali kwa wapinzani hao, anaandika Mwandishi Wetu.

Wanachama hao waliojiunga na CCM leo katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) unaofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, ni Prof. Kitila Mkumbo, Wakili Albert Msando, Samson Mwigamba waliotoka ACT-Wazalendo na Laurance Masha na Patrobas Katambi waliokuwa CCM.

Hizi hapa kauli 11 ambazo zimetolewa na wanachama hao wapya walipopewa nafasi ya kuzungumza na wajumbe wa NEC wa CCM waliokuwa katika mkutano huo walipokuwa wanatambulishwa.

1. “Katika siku za hivi karibuni tumeona mapinduzi ya kiutawala, kiitikadi, kiuchumi” – Dk. Mkumbo
2. “CCM ndio chama pekee kinachoonekana kina nguvu hapa nchini” – Dk. Mkumbo
3. “Nimekubali kurudi kwa dhati, ninaomba ridhaa nirudi mnipokee” – Lawrence Masha
4. “Nimerudi zizini nikiwa na mkia, nipo tayari kutumika” – Lawrence Masha
5. “Yale tuyotarajia Wapinzani tuyaone yakifanyika, yanafanyika katika utawala wako Rais Magufuli, tuna kila sababu ya kukuunga mkono” – Samson Mwigamba
6. “Kadri wanavyopiga kelele, ndivyo wewe unazidi kupanda mlima” – Samson Mwigamba
7. “CCM ni chama kinachoonyesha kuwajali watu, mimi kama kijana ninajivunia kuwa Mwanachama wa CCM” – Alberto Msando
8. “CCM kilihaidi kupambana na umaskini, kutengeneza ajira, kurudisha nidhamu na uwajibikaji. Tuna kila sababu ya kupongeza kwa haya mambo mazuri” – Alberto Msando
9. “Leo hii nasaliti ubinafsi, umimi kwa kuamua kujiunga na CCM” – Patrobasi Katambi
10. “Upinzani wa leo unajadili mambo binafsi na matukio kuliko kujadili namna ya kulisaidia Taifa” – Patrobas Katambi
11. “Kijana ndani ya upinzani ni karai linalojenga ghorofa. Karai huonekana takataka baada ya ghorofa kukamilika” – Patrobasi Katambi

1 Comment

  • HOJA GANI SASA HIZI AU MWANA HALISI NA NYIE MMEJIUNGA NA CCM , HAPO KUNA HOJA SASA?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!