May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Katibu Tawala Arusha afariki ajalini

Spread the love

 

KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha (RAS), Richard Kwitega, amefariki dunia leo Jumatano saa 9:30 alasiri, tarehe 3 Februari 2021, katika ajali ya gari eneo la Mdori, Wilaya ya Babati, mkoani Manyara. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Ajali hiyo, imehusisha gari lake na basi la abiria, ambapo Kwitega alikuwa anakwenda jijini Dodoma kikazi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawaza za Mikoa na Serikali za MItaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema, mareemu Kwitenga, aliteuliwa na Rais John Magufuli kuwa RAS, tarehe 25 Aprili 2016.

Amesema, kabla ya uteuzi huo, aliwahi kufanya kazi katika mikoa mbalimbali nchini na “Serikali inatambua na itaendelea kuenzi mchango wa marehemu Richard Nkingwa Kwitega katika ujenzi wa Taifa letu.”

Waziri Jafo amesema, taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi zitaendelea kutolewa na uongozi wa mkoa wa Arusha.

Mapema leo asubuhi, Kwitenga alifungua mkutano mkoani humo na kuwaaga washiriki kwamba anakwenda Dodoma kikazi.

error: Content is protected !!