Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Katibu Mkuu NCCR Mageuzi amvaa Mbatia, ashusha shutuma nzito
Habari za SiasaTangulizi

Katibu Mkuu NCCR Mageuzi amvaa Mbatia, ashusha shutuma nzito

Martha akiwa na Mbatia
Spread the love

MGOGORO ndani ya Chama cha NCCR Mageuzi umeendelea kufukuta baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Martha Chiomba kuibua na kudai maisha yake yapo hatarini kutokana na kuwindwa na kundi la vijana aliloliita ‘genge la wahuni’. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Pia amedai aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia alimuita nyumbani kwake akiwa pamoja na viongozi wengine wawili kisha kumshinikiza kujiuzulu ilihali wakitambua kuwa alikuwa anaumwa na ametoka kufanyiwa operesheni kubwa ya tumbo. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Amesema chanzo cha mgogoro kati yake na Mwenyekiti huyo, ni kitendo cha yeye kukataa kujiuzulu nafasi hiyo ambayo alipata fununu kuwa Hamad Masoud aliyejiengua ACT Wazalendo baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Uenyekiti wa Taifa, alitakiwa kuja kuchukua nafasi Katibu Mkuu NCCR Mageuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 29 Mei, 2022 jijini Dar es Salaam, Chiomba amesema anashangaa kusiki Mbatia ndiye analalamika kutishiwa maisha wakati yeye (Chiomba) halali nyumbani bali analala kwa ndugu.

Akisimulia matukio hayo Chiomba amesema tarehe 17 Februri, 2022 aliitwa nyumbani kwa Mbatia na kuwakuta yeye pamoja na viongozi wawili wa chama ambaye ni Mustapha Muro na Hemed Musabaha.

“Mwenyekiti akachukua simu yangu na kuiweka anapojua kisha akaniambia kuna vijana wananitaka mimi Katibu Mkuu ujiuzulu, wametuma barua kwenye mitandao ya kijami.

“Nilishangaa kuwa kama kuna tatizo lolote kuna vyombo ndani ya chama ambavyo tumejiwekea, kuna utaratibu ambao unafuatwa, ila hiyo haikutosha, nikaambiwa ili kulinda heshima yako unatakiwa ujiuzulu.

“Nikawauliza kwani kazi za chama ni zipi, hasa ikizingatiwa natekeleza majukumu yangu inavyotakiwa? malumbano yalikuwa makali zaidi, mmoja wao aliendelea kunishambulia kwa maneno ya kunishambulia,”amesema Katibu Mkuu huyo na kuongeza;

“Nikajiuliza kwanini niitwe mwenyewe tena mwanamke alafu wanaume watatu wananishinikize nijizulu, wakaniambia nijiuzulu kwa kuandika barua, nikahoji mmoja aliandika mwenyewe, mwingine aliandikiwa, hawakufikiria afya yangu maana niliitwa nikiwa natoka hospitali. Nikawaambiwa niandikie hiyo barua.

“Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama alisema angeniandikia, niliambiwa nisimueleze mtu yeyote kulinda heshima,” amesema.

Amesema aliwashirikisha makamu mwenyekiti Zanzibar na aliyekuwa Naibu Katibu, Anthony Komu na Peter Bakana ambao walimshauri asijiuzulu.

“Nikawaambia utaratibu unaonekana sio sahihi kwa sababu kwanini niitwe nyumbani kwa mwenyekiti, wangetakiwa kuniita kwenye mkutano mkuu.

“Lakini inaonesha nyuma ya pazia kulikuwa ndugu Hamad Masoud aliyekuwa ametoka ACT Wazalendo… walitaka aje wampe nafasi yangu,” amesema.

Amesema Mbatia baada ya kupata taarifa hizo za kugoma kujiuzulu, alimuuliza kwanini amemueleza Komu kama alikuwa amepanga kubadilisha mawazo.

“Mwenyekiti aliniambia kwanini nimekwenda kwa Komu kama nimebadilisha mawazo badala ya kwenda kwake, nikamjibu hii nafasi sijapewa na kikundi cha watu, nilichaguliwa na mkutano. Jumapili hakuja… na hapo ndipo ugomvi uliopoanzia,” amesema.

Ameongeza kuwa anajua Mbatia hajafukuzwa bali amesimamishwa.

“Yeye ndio anatuletea wahuni ndani ya chama, huwezi kuahirisha mkutano unavyotaka wewe, asubiri mkutano ujao atajitetea, asikanushe kuwa hajawahi kunilazimisha nijiuzulu kwa sababu sipelekeshwi hovyohovyo, nimegoma.

“Najua nilichofanya ni kigumu, ninaweza kuuawa kwa risasi au chochote ila nitasimamia misingi usawa na demokrasia ya kweli,” amesema.

Akizungumzia mkutano mkuu ambao ulikifuta kikao cha tarehe 21 Mei, mwaka huu amesma mkutano huo haukufutwa bali yalikuwa matakwa ya wachache waliokuwa na ajenda zao.

Amedai kuwa ndani ya chama hicho kuna unyanyasaji mkubwa na walikuwa na malengo ya kumuonea ndio maana wakamuita yeye mwanamke mwenyewe na kumshinikiza kujiulizu.

Pamoja na mambo mengine amedai kuwa kuna kikundi kilichoundwa kwenye group la Whatsap ambacho kimetumika kumtukana kiasi cha kumsababishia operesheni yake aliyofanyiwa kupasuka.

Amedai licha ya viongozi wote akiwamo Mbtai kuwepo kwenye kundi hilo , hakuwakemea vijana hao waliokuwa wakimvua nguo Katibu Mkuu.

Kutokana na hali hiyo amesema tayari amechukua RB kwa ajili ya kwenda kuwashtaki vijana hao kwa sababu ushahidi anao.

Hata hivyo, aligoma kutaja tuhuma anazokabiliwa nazo, ikiwa ni pamoja na tuhuma alizotaja idadi kuwa ni 14 za Mbatia zilizosababisha avuliwe uenyekiti.

Hivi karibuni Mbatia alizungumzia na vyombo vya habari na kudai kuwa maisha yake yapo hatarini kutokana na chuki uliyoenezwa na wanasiasa wenzie kuwa alipewa Sh milioni 500 kuisaliti NCCR Mageuzi kipindi cha utawala wa Rais John Magufuli.

Kuhusu unyanyasaji wa kijinsia Mbatia alikanusha kuwa na chumba maalum kinachotumika kuteka watu au kwa vikao maalumu na kufanyia ukatili wa kijisnia nyumbani kwake.

Aliomba vyombo vya dola kwenda nyumbani kwake kwenda kuchunguza chumba hicho cha kunyanyasaji wanawake nyumbani kwake.

Wiki iliyopita Mbatia alisimamishwa uenyekiti wa chama hicho katika Mkutano mkuu wa chama hicho ambao licha ya kudai ulikuwa batili, lakini Msajili wa vyama vya siasa nchini ameubariki kuwa ulikuwa mkutano halali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!