Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Katibu Mkuu CCM awataka wahitimu vyuo vikuu wasichague kazi
Elimu

Katibu Mkuu CCM awataka wahitimu vyuo vikuu wasichague kazi

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo
Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, ametoa wito kwa vijana wanaohitimu vyuo vikuu, wafanye shughuli nyingine za kujitafutia kipato ambazo ziko nje ya taaluma walizosomea. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).

Chongolo ametoa ushauri huo leo tarehe 27 Februari 2023, katika ziara yake ya kikazi mkoani Singida.

Mbali na ushauri huo kwa wahitimu wa vyuo vikuu, Chongolo amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika vyuo vya elimu na ufundi stadi (VETA), kwa ajili ya kujiongezea ujuzi wa kujiari, badala ya kuwaacha vijiweni.

“Vijana wengi wakishamaliza vyuo akiwa na digrii ya ualimu, haamini kama anaweza kuwa na uwezo wa kufanya kitu kingine nje ya taaluma aliyonayo. Tunajenga vyuo vya VETA kote nchini lengo kusogeza elimu ya ujuzi karibu na wananchi, pelekeni vijana waende wakasome na kupata ujuzi kwani utawapa uhakika wa kujiajiri na kujitafutia shilingi,” amesema Chongolo.

Aidha, Chongolo amewataka viongozi wa Serikali ngazi ya wilaya, kuanzisha program za kuwapelekea VETA vijana walioko katika maeneo yao.

1 Comment

  • @THINK/Dedication/Remember”@ EMPLOY/US THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 32.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love  HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari...

error: Content is protected !!