Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Katibu CCM asimamishwa kwa rushwa, Magufuli asema…
Habari za SiasaTangulizi

Katibu CCM asimamishwa kwa rushwa, Magufuli asema…

Katibu wa Itikadi na uenezi CCM, Shaka Hamidu Shaka
Spread the love

 

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamidu Shaka, amesimamishwa kazi na chama hicho, kupisha uchunguzi wa tuhuma za kula rushwa kutoka kwa madiwani wakati wa mchakato wa upatikanaji wa meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi tarehe 11 Februari 2021, na Rais wa Tanzania, John Magufuli, wakati anazindua Soko Kuu la Mkoa wa Morogoro.

Licha ya kutomtaja jina, Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa, amesema, Shaka atajadiliwa kwa tuhuma za kula rushwa za madiwani.

“Na bahati mbaya, hata utafutaji wa meya hapa ulijaa rushwa ndio maana katibu wa CCM hapa tumemsimisha kazi, atajadiliwa kwa sababu alikula rushwa kwa madiwani,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alitoa taarifa hiyo wakati anazungumzia upatikanaji wa meya wa manispaa hayo, Pascal Kihanga, ambapo amesema hakustahili kuwa Meya wa Manispaa ya Morogoro.

Rais John Magufuli

Kiongozi huyo wa CCM Taifa, amesema aliyestahili kuwa meya wa manispaa hiyo hamkurudisha, hivyo amemuagiza Kihanga kusimamia wananchi waliomchagua.

“Na wewe mstahiki meya nataka ubadilike, najua umeupata umeya wa bahati bahati hapa, mimi napenda kuzungumza ukweli. Nasema uongo ndugu zangu? Hukutakiwa kuwa meya, aliyetakiwa sikumrudisha kuwa meya,” amesema Rais Magufuli.

Madiwani wa Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro, walifanya uchaguzi wa meya tarehe 23 Novemba 2020, ambapo majina mawili yalifungana kwa zaidi ya mara tatu, baada ya kura zao kufanana kila walipopigiwa.

Baada ya majina hayo kufungana, uchaguzi huo ulirudiwa tarehe 1 Disemba 2020, ambao pia walifungana kwa kupata kura 21 kila mmoja.

Madiwani waliofungana walikuwa ni Seifu Chomoja na Paschal Kihanga, ambapo majina yao yalipelekwa katika Kamati Kuu ya CCM Taifa, ambayo ilirlirudisha jina la Kihanga.

1 Comment

  • Je TAKUKURU IMEHUSISHWA katika kesi hii ya rushwa? Au kwa sababu ni CCM kwa hiyo Takukuru haihusiki?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

BiasharaTangulizi

TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari

Spread the love  CHAMA cha wanasheria Tanzania (TLS), kimejitosa katika sakata la...

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

error: Content is protected !!