July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Katiba yawasumbua mpira wa mikono

Spread the love

CHAMA cha mpira wa mikono Tanzania (TAHA) kimetakiwa kufuata sheria na taratibu za usajili wa katiba wanayoitaka kama walivyoagizwa na Msajili wa vyama vya michezo nchini, anaandika Aisha Amran.

Rai hiyo imetolewa leo na Allen Alex afisa michezo mkuu kitengo cha usajili wa vyama vya michezo kufuatia malalamiko ya chama hicho kwa vyombo vya habari kuhusu kunyimwa usajili wa katiba mpya ya chama chao.

Amesema wakati chama hicho kinawasilisha barua ya kuomba usajili katiba aliwapa utaratibu wa kufuata katika usajili ambao kwanza ni kurudisha cheti cha mwanzo cha katiba ya zamani pamoja na orodha ya mabadiliko wanayotaka kufanya.

Aidha chama hicho kinatakiwa kufanya mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba chini ya sheria ya usajili wa vyama vya baraza la michezo la taifa (BMT) ambayo inaeleza ni lazima mkutano kuwa na wajumbe wa vyama vya michezo kutoka mikoa isiyopungua 13 ya Tanzania bara.

Amebainisha kutokana na masharti hayo chama hicho hakikuweza kutimiza na badala yake wakafanya mkutano na wajumbe ambao sio sahihi kisheria.

Allex amesema Desemba 17 mwaka jana, chama hicho kiliwasilisha barua ya kuomba usajili wa katiba mpya ambayo ilikuwa inataka kubadilisha jina la chama hicho kutoka Tanzania Ameteur Handball Association (TAHA) na kujulikana kama shirikisho la mpira wa mikono Tanzania(THI).

error: Content is protected !!