Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Katiba pendekezwa itachochea Wazanzibar kudai uhuru’
Habari za Siasa

‘Katiba pendekezwa itachochea Wazanzibar kudai uhuru’

Othamn Masoud Othman, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
Spread the love

OTHMAN Masoud Othman, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kabla ya kutimuliwa kwa kuunga mkono mapendekezo ya serikali tatu, amesema Katiba inayopendekezwa  itajenga mfumo utakaosababisha kizazi kijacho cha Zanzibar kidai uhuru badala ya haki ndani ya Muungano, anaandika Pendo Omary.

Othman alifutwa kazi na Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na Said Hassan Said baada ya kumalizika kwa Bunge Maalum la Katiba 2014, ambapo alipiga kura ya wazi ya kuunga mkono mapendekezo ya serikali tatu kinyume na msimamo wa chama tawala.

Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa kitaifa wa Katiba uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Othman amesema;

“Kwa ujumla Katiba inayopendekezwa sio tu kwamba imerasimisha kero za Muungano lakini inajenga mfumo utakaofanya kizazi kijacho cha Zanzibar kidai uhuru badala ya haki ndani ya Muungano.”

Amesema katika kujenga mustakbali wa kikatiba ndani ya Tanzania, suala la Muungano haliwezi kuepukwa kuwa ajenda kubwa na ya msingi.

“Taifa letu limepata uzoefu wa kutosha wa kasoro za Muungano.  Ni dhahiri kuwa itikadi na kutokuwepo upeo na uthabiti katika kujenga mfumo mpya wa kikatiba kumesababisha Katiba inayopendekezwa kuwa mbaya na dhaifu zaidi, katika kujenga mustakbali huo,” amesema Othman.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!