May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Katiba mpya: Mbowe atangaza J’mosi kuvaa sare za Chadema

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

 

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani, Tanzania- Chadema amesema, Jumamosi zote kuanzia kesho, tarehe 12 Juni 2021, atakuwa akivaa sare za chama hicho hadi nchini hiyo ipate Katiba Mpya. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Mchakato wa Katiba Mpya, uliishia kwa Katiba Pendekezwa ambapo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), tarehe 2 Aprili 2015, ilitangaza kuahirishwa kwa kura ya maoni ya katiba hiyo.

Kura hiyo ya maoni, ilikuwa ifanyike tarehe 30 Aprili 2015, lakini iliahirishwa kutokana na kutokamilika kwa uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR).

Leo Ijumaa, tarehe 11 Juni 2021, Mbowe ametumia ukurasa wake wa Twitter kuitangaza Jumamosi kuwa siku ya mavazi ya chama hicho.

“Kesho & kila J’mosi nitavaa sare za chama chetu Chadema hadi TZ ipate Katiba Mpya.”

“Azimio hili limependekezwa & kuungwa mkono & Vikao & Mikutano yote inayoendelea nchini. Wanachadema wote tuungane, tutambuane, tukilinde Chama & tutetee Uhuru na Haki popote tulipo. Umoja ni nguvu!” ameandika Mbowe aliyeanza kukiongoza chama hicho tangu mwaka 2004.

error: Content is protected !!